Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Alix Michel.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ), katika Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016.
Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kwa lengo la kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC katika Uchaguzi wa Shelisheli utaofanyika tarehe 8 - 10 Septemba, 2016.
Wajibu huu wa Tanzania katika kuongoza misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa chaguzi za kidemokrasia katika Kanda ya SADC. Akiwa nchini Shelisheli, Mheshiwa Mahiga (Mb), alizindua rasmi misheni hiyo tarehe 2 Septemba, 2016 kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Magufuli. Misheni hiyo ya waangalizi itakua na waangalizi kutoka nchi za SADC .
Wakati akiwa nchIni Shelisheli, Mheshimiwa Waziri Mahiga alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. James Alix Michel Rais wa Sheliseli .
Pia Mheshimia Waziri Mahiga aliweza kufanya mazungumzo na Mhe. Joel Morgan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Seychels na kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Seychels.
Imetolewa na :
BALOZI INNOCENT E. SHIYO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akimtambulisha Balozi Innocent Shiyo kwa Rais wa Shelisheli, Alix Michel
Rais wa Shelisheli, Alix Michel akiwa kwenye kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Baloz Dk. Augustine Mahiga nchini Shelisheli.
Waangalizi wa uchaguzi wa wabunge wa Shelisheli katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga na Balozi Innocent Shiyo. (Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).
No comments:
Post a Comment