Friday, December 20, 2013

DAWA ZA KULEVYA: UNYAMA WA KUTISHA WAFANYIWA WATANZANIA


Sakata la Watanzania wanaoshikiliwa nchini Pakistan na mtandao unaohusika na biashara ya dawa za kulevya ambao wapo mafichoni nchini humo kama dhamana ya vigogo wanaofanya biashara hiyo nchini, limechukua sura mpya.

Mmoja wa vijana kutoka Tanzania akiwa kifungoni
Taarifa zilizolifikia gazeti hili, zinasema idadi ya Watanzania wanaopelekwa nchini humo na vigogo wa biashara hiyo nchini inazidi kuongezeka ambapo hivi karibuni, vijana wawili wote raia wa Tanzania, nao wamepelekwa nchini humo.

Awali vijana hao walikuwa wakiishi katika nchi za Nigeria na Afrika Kusini ambapo kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka Pakistan (jina tunalo), ambaye naye anashikiliwa nchini humo na mtandao huo, alisema wapo Watanzania wengine wanne ambao wameingia katika jumba la mateso.

Alisema Watanzania hao huifadhiwa katika jumba hilo kama dhamana ya vigogo wa biashara hiyo nchini ambao hutumiwa dawa za kulevya na kuingia nchini bila wao kujua chochote.

"Kati ya Watanzania hao, wawili wamepelekwa katika Mji wa Turbat kama dhamana ya vigogo wanaonunua sawa za kulevya Pakistan ili waweze kulipa madeni kwa wakati.

"Yupo Mtanzania anayeitwa Said, mkazi wa Temeke, Dar es Salaam ambaye vigogo husika walimshawishi kuja huku akiwa Afrika Kusini, aliporudi Tanzania walimsafirisha na sasa yupo chini ya ulinzi, miguu na mikono imefungwa minyororo (PICHANI JUU).

SOMA ZAIDI...

"Tunaomba mtusaidie kwani tupo Watanzania wengi na wengine wanazidi kuletwa bila kuambiwa wanakuja kufanya nini...huku ukiingia kutoka ni ngumu," kilisema chanzo chetu.

Aliongeza kuwa, kigogo aliyemsafirisha kwenda nchini humo (jina tunalo), amemkimbia na hivi karibuni alimtumia ujumbe wa matusi katika simu yake (sms), akisema haiogopi Serikali,
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP wala vyombo vya habari.

Ujumbe huo ulikuwa ukisomeka kuwa; "Biashara ya unga haiusiani na polisi wala waandishi wa habari, nenda kokote, siogopi Serikali na hakuna anayenitisha akiwemo IGP, situmi
hela na sina utajua mwenyewe...fanya uwezalo na mimi sipo Tanzania, wambie wanitafute kama watanipata," ujumbe huo ulisomeka hivyo.

Aliongeza kuwa, amefikia uamuzi wa kuomba msaada wa Serikali na vyombo vya habari baada ya kumbembeleza sana kigogo huyo kupitia kwa mkewe na ndugu zake akimuomba
wamalizane na matajiri wa Pakistan ili wamuachie.

Alisema hivi sasa, uwepo wao katika jumba hilo wanaishi kwa kuwaongopea matajiri hao kuwa wanaendeleza mawasiliano na familia zao ili walipe madeni wanayodai na kuwaachia.

"Familia yangu ikienda kwa kigogo aliyenisafirisha, wanapewa ahadi hewa na kuondoka na sasa wamewakimbia kabisa hivyo hawana jinsi ya kumpata kigogo husika," alisema.

Aliitaka Serikali ifahamu kuwa, nchi ya Pakistan ndio inayoingiza dawa hizo kwa wingi nchini kwani matajiri wakubwa nchini humo hutegemea biashara hiyo.


No comments:

Post a Comment