Wednesday, December 18, 2013

BALAA: UTAMU WA NGONO WAMUUA

Mwanaume mmoja nchini Malawi alizimia na kisha kufariki wakati akifanya tendo la ngono na changudoa, imedaiwa kifo chake kimesababishwa na utamu wa ngono.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa jeshi la polisi nchini Malawi, Edna Logowe(Pichani Kulia) alisema Bw. Fletcher Jere alikumbwa na mkasa huo baada ya kuchukua malaya hivi karibuni katika mitaa ya Ndirande ya jijini Blantyre ili “kukata kiu yake”

Kwa mujibu wa magazeti ya nchini humo, inaripotiwa kuwa Fletcher alizirai gafla na kudondoka toka kitandani baada ya mambo kukolea akiwa na Malaya huyo.

Msemaji huyo wa polisi aliliambia gazeti la Daily Times la nchini humo “Jere alikumbwa na mauti sababu ya kuzuduwa utamu wa ngono”

SOMA ZAIDI...

“Malaya huyo hatofunguliwa mashtaka sababu hajafanya kosa lolote sababu ya kuwa mtamu katika tendo hilo” aliongeza Bi. Logowe.

Wataalamu wamedai kifo cha Jere kinaweza kuwa kimesababishwa na mshtuko, tukio ambalo lilisababisha moyo kushindwa kusukuma damu kwenye sehemu nyingine za mwili. Hii inaweza kusababishwa na “mwenendo mbaya wa mapigo ya moyo”

Inawezekana kabisa Jere ana matatizo ya mshtuko wa moyo





No comments:

Post a Comment