Ndege hiyo ilikuwa itue kwenye Uwanja wa Kimataifa
Kilimanjaro, lakini ilitua kwenye uwanja wa Arusha ambao njia ya kutua ndege
kwenye uwanja huo inasemekana ni urefu wa mita 1.620 tu, au futi 5.315. Uwanja
huo hauna uwezo kumudu ndege kubwa kama hiyo aina ya Boeing 767.
Kumekuwepo na maswali mengi kuhusiana na ndege hiyo
kutua katika uwanja huo kwani ni hatari kwa ndege kubwa kama hiyo kutua kwenye
uwanja mdogo kama huo.
Uwanja huo, ambao kuinuliwa kwake kumo kwenye hati
maalum zinazoonesha ni futi 4.550 juu ya usawa wa bahari au mita 1.387.
Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari, ndege hiyo
iliyokuwa imesajiliwa kama ET-AQW ilikuwa kwenye safari namba ET815 kutoka
Addis kupitia Kilimanjaro kwenda Zanzibar na kurudi Addis Ababa, Ethiopia.
Taarifa za awali, zilieleza kuwa hakuna abiria wala
mfanyakazi yeyote aliyejeruhiwa na kwamba ndege hiyo ilisimama kabla ya kufika
mwisho wa njia ya kutua.
Uwanja huo pia unaripotiwa kufungwa kutoruhusu
ndege kuingia wala kutoka kutokana kupangwa upya kwa safari za ndege za
Precision Air na ndege nyingine zinazotoka na kwenda mbuga za wanyama.
Vyanzo vya habari kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro viliongeza kusema kwamba ndege hiyo ilikuwa itue
kwenye uwanja huo, lakini haikuwezekana kwa sababu kulikuwepo na ndege nyingine yenye hitilafu
kwenye njia ya kutua ndege.
Ndege hiyo kwenda kutua Arusha imekuwa mjadala
mkali miongoni mwa wadau wa safari za ndege nchini, kwani abiria, wafanyakazi
na ndege yenyewe walikuwa hatarini.
Bado haifahamiki kama ndege hiyo, B767, hata kama
itaondolewa vifaa na siti, itaweza kuruka salama kutoka uwanja wa Arusha kwenda
Kilimanjaro, wakati uwanja huo utakapokuwa umefunguliwa na shughuli kuanza
tena.
No comments:
Post a Comment