Thursday, December 19, 2013

KIGOGO WA WAHAMIAJI HARAMU AKAMATWA

Watu wawili akiwemo raia wa Burundi, Nduwayesu Pail, wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kuhusika na usafirishaji wa wahamiaji haramu kinyume na sharia.

Nduwayesu Paul (31), ambaye naye yuko nchini kinyume cha sheria,anadaiwa kuhusika katika matukio ya usafirishaji wahamiaji haramu na kuwaingiza nchini kwa kupitia njia za panya kwa kushirikiana na raia wa nchini Tanzania.

SOMA ZAIDI...

Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watu hao, Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Johannes Msumule, alisema watu hao ambao ni raia wa Burundi na Mtanzania mmoja mkazi wa Rombo mkoani hapa, walikamatwa Desemba 17, mwaka huu saa 7:15.

"Raia huyu wa Burundi kwa taarifa za awali inaonesha kuwa yuko nchini isivyo halali na anafanya kazi isivyohalali, na hayupo peke yake, yupo na kaka yake ambaye anatafutwa ndani na nje ya nchi, ambaye naye yupo katika mtandao huu wa kusafirisha wahamiaji haramu, hawa ni watu hatari sana, na ni lazima tuwashughulikie kikamilifu," alisema Msumule.

Msumule alisema raia huyo wa Burundi Nduwayesu na Leokadia Tarimo (54) ambaye ndiye mmiliki wa nyumba ya kulala wageni ya Impala, walikutwa na raia hao wa Ethiopia 10 wakiwa wamewahifadhi katika nyumba ya kulala wageni.

Alisema kukamatwa kwa watu hao kumewasaidia sana kufahamu mtandao wa usafirishaji wahamiaji haramu na kuwaingiza nchini kinyume cha sheria.

Alisema maofisa wa Uhamiaji walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kunauwepo wa watu wasio waelewa katika gesti ya Impala na ndipo walipofika katika nyumba hiyo na kufanya ukaguzi.


No comments:

Post a Comment