Thursday, March 30, 2017
UCHACHE WA MATUMIZI YA BENKI HUCHANGIA KUCHAKAA HARAKA KWA FEDHA
Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M. Dollah, akitoa mada juu ya Huduma za Kibenki Benki Kuu ya Tanzania 
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
IDADI ndogo ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki kunachangia pakubwa kuchakaa haraka kwa fedha.
Hayo yamesemwa na Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M.Dollah, wakati akijibu maswali ya Washiriki wa Warsha ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, inayoendelea kwenye ukumbi wa BoT tawi la Zanzibar, leo Machi 30, 2017 waliotaka kujua ni kwa nini fedha za noi zinachakaa haraka hususan shilingi 500 na shilingi 1,000/_
“Ubora wa karatasi zinazotumika kutengenezea noti zetu unalingana, lakini matumizi makubwa ya noti hizo zilizotajwa, zinapita kwenye mikono ya idadi kubwa ya watu na hivyo kupelekea kuchoka haraka.” Alifafanua
Akifafanua zaidi alisema, Idadi ya Watanzania kwa sense iliyofanyika mwaka 2012 ni Milioni 48, lakini kati ya hao ni Watanzania Milioni 4 tu ndio wanatumia huduma za kibenki, (kuwa na akaunti benki), na idadi ya waliosalia, hutunza wenyewe fedha hizo.
Utunzaji mbaya wa fedha na hali ya hewa ya baadhi ya maeneo nchini, huchangia kuchakaa haraka kwa fedha “ Kwa mfano, kule Tanga maeneo ya Lushoto na Kibondo mkoani Kigoma, kutokana na rangi ya udongo wa sehemu hizo, utakuta fedha inachakaa haraka sana, alisema Bw.Dollah.
Akielezea majukumu ya Kurugenzi ya Huduma za Kibenki ya Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Dollah alisema, Sheria namba Nne (4) ya BoT, imeipa kurugenzi hii jukumu la kusanifu, kutoa, kusambaza na kuharibu fedha,(noti na sarafu), zilizochakaa.
Wednesday, March 29, 2017
WANANCHI BINAFSI WANAWEZA KUKOPA (MOGEJI) MORTGAGE KATIKA MABENKI

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WANANCHI binafsi wanaweza kwenda kwenye mabenki na kuomba mikopo ya fedha za ujenzi, (Mortgage Finance), bila ya kuanza kupitia kwenye taasisi nyingine za fedha.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi-Usimamizi wa Mabenki Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Eliamringi Mandari, (pichani juu), wakati akiwasilisha mada juu ya utaratibu wa mikopo ya fedha kwa ajili ya ujenzi, (Mortgage Finance) na utunzaji taarifa mteja (mkopaji) katika kitunza taarifa cha kibenki, (Databank) kwenye semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha leo Machi 29, 2017 inayoendelea kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (tawi la Zanzibar), mjini Unguja.
“Watu wengi hawajui kama kuna fursa hii ya ku-mortgage, kwa maana ya kujenga, kununua au kurekebisha nyumba yako, na katika kudhamiria kufanya hayo, benki inaweza kutoa masharti ambayo ni ya kurejesha fedha (mkopo) huo kwa muda mrefu kati ya miaka 5 hadi 20.” Alisema.
Hata hivyo alisema kama ilivyo kwa masharti mengine yahusuyo kukopa, hata fursa hii ya kukopa fedha kwa ajili ya ujenzi vigezo na masharti pia huzingatiwa ili benki iweze kutoa mkopo huo.
Aidha kuhusu mfumo wa taarifa unaosaidia mkopeshaji,(lender), kumjua mkopaji, (borrower), ujulikanao kama, Credit Reference System, (DBS), alisema Sheria namba 48 ya BoT kuhusu masuala ya kubadilishana taarifa za mikopo, kwa mabenki na taasisi nyingine za fedha inalazimisha mabenki na taasisi hizo kutuma taarifa za wateja (wakopaji), kwenye Databank ya BoT kila mwezi, alisema Bw. Mandari
MTANZANIA ALIYEWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA MUDA MFUPI AMUANGUKIA WAZIRI MWAKYEMBE

Gaudence Lekule akiwa katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro baada ya kukimbia kwa muda wa wa saa 8:36 mpya akiwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza kutumia muda huo kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro na kushuka.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MTANZANIA ,Gaudence Lekule (31) anayeshiriki michezo ya kupanda milima kwa kasi (Mountain Run) amemuomba Waziri mpya wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo ,Dkt Harison Mwakyembe kutupia jicho michezo mingine kwani ina nafasi kubwa ya kutangaza na kuletea sifa taifa.
Lekule anayeshikilia rekodi ya kuwa Mwafrika wa kwanza Duniani kupanda kwa muda mfupi katika Mlima Kilimanjaro akitumia muda wa jumla wa saa 8:36 alitoa wito pia kwa kampuni,taasisi binafsi na za serikali kujitokeza kudhamini wanamichezo kutokana na eneo hilo upo uwezekano wa kujitangaza zaidi kidunia.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum,Gaudence alisema kwa sasa yupo katika maandalizi ya kuweka rekodi mpya katika milima mirefu na maarufu Duniani kwa kufanya mazoezi ya awali hapa nchini na baadae nje ya nchi.
“ Nashukuru kuitangaza Tanzania kidunia na tayari nimepata mialiko mingi ya kwenda nje kushiriki mashindano ya Mountain Run ,Lengo langu ni kuweka rekodi katika milima mirefu duniani hivyo bado naendelea na mazoezi na nitaendelea kufanya mazoezi hapa kwetu na badaae nje ya Tanzania”alisema Gaudence .
Alisema hadi sasa rekodi ya Dunia inashikiliwa na raia wa nchi ya Ecuador, Karl Egloff aliyetumia muda wa saa 6:53 kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro ,rekodi aliyoweka mwaka 2014 akivunja rekodi ya Kilians Jornet raia wa Hispania aliyetumia muda wa saa 7:20 kupanda na kushuka mlima Kilimanjaro mwaka 2010.
Lekule alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni mabadiliko hali ya hewa inayochangia kushindwa kufanya mazoezi na upatikanaji wa mahitaji kama chakula pamoja na mavazi kwa ajili ya mchezo huo unafanyika kuanzia urefu wa mita 3500 hadi 5800.
Tuesday, March 28, 2017
BOT YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI ZA UCHUMI NA FEDHA

Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, akiwasilisha mada juu ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania, wakati wa semina ya Wiki moja kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, tawi la Zanzibar, leo Machi 28, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUMUKO wa bei utokanao na ongezeko la Fedha ni hatari sana katika uchumi wa nchi, Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, ameiambia semina ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kutoka vyombo mbalimbali vya habari leo Machi 28, 2017.
Semina hiyo ya wiki moja inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar, ina lengo la kuwaelimisha waandishi wa habari kuhusu namna bora ya uandishi w ahabari za uchumi na fedha.
Chini ya Sera ya Fedha, (Monetary Policy), Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kama mtengeneza fedha (mchapishaji), inaweza kudhibiti mfumuko wa bei utokanao na ujazi wa fedha kutokana na viashiria vya uwezo wa uzalishaji katika taifa unapopungua au kuonegzeka. Sera ya fedha maana yake ni pale Benki Kuu inapoamua kuongeza fedha kwenye mzunguko au kupunguza na hii itategemea sana na uzalishaji bidhaa, alifafanua Lusajo.
“Inapogundulika kuwa kiwango cha fedha ni kikubwa kwenye mzunguko kuliko uzalishaji BoT kazi yake hapa ni kupunguza fedha kwenye mzunguko na hii sio kwa eneo fulani tu la nchi bali ni nchi nzima ambako fedha ya Tanzania inatumika.” Alisema Mchumi huyo.
Monday, March 27, 2017
PPF YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA LONGIDO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo,(wanne kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Afya), Dkt. Zainabu Chaula,(kulia), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Daniel Chongolo, (wapili kushoto), na viongozi wengine, wakiangalia kitanda cha kujifungulia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na PPF.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kushoto), Viongozi wa Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido, wakitembelea wodi ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Longido, ambapo ni moja kati ya vituo vilivyonufaika na msaada huo wa vifaa tiba kama sehemu ya mchango wa PPF kwenye Jamii.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PPF, umekabidhi vifaa tiba katika Mkutano wake wa 26 wa Wanachama na Wadau. Vifaa tiba hivyo vyenye jumla ya shilingi 99,983,700/- vilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa PPF.
Msaada huo utatolewa katika hospitali na vituo vya afya 16 nchini kama mchango wa PPF kwa shughuli za kijamii.
Wakati wa kufunga Mkutano huo, mgeni rasmi Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu aliungana na Bodi ya Wadhamini wa PPF, Menejimenti na baadhi ya Wafanyakazi wa PPF walienda kukabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha Afya, Longido, ambacho ni moja kati ya vituo vya Afya 16 nchini vitakavyonufaika na msaada wa vifaa hivyo.
Mhe. Jenista Mhagama, alisema, PPF imefanya jambo zuri la kusaidia Jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwapatia huduma bora za afya wananchi wake.
“Hivi sasa akina mama wa Longido, mtajifungua katika mazingira mazuri nimeona kati ya vifaa tiba vilivyotolewa leo ni pamoja na kitanda cha kujifungulia hongereni sana PPF.” Alisema Mhe. Mhagama.
WAZIRI MWIGULU AWAASA ASKARI KUTOWABAMBIKIZIA WATU KESI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Mzee John Samwel Malecela akizungumza wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/VikosiNa Mathias Canal, Dodoma
Askari na Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wameaswa kutotumia madaraka yao vibaya kwa kuwabambikizia wananchi kesi kwani kufanya hivyo ni kushindwa kusimamia dhamira njema ya Mhe Rais ya kuwapatia wananchi wanyonge haki zao stahiki.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe Mwigulu Nchemba wakati akifungua kikao cha kazi cha Siku tatu cha mwaka 2017 kwa maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mjini Dodoma.
Mhe Mwigulu amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kuwabambikizia kesi, Kuwabadilishia watu kesi zao za msingi kwa sababu ya kushindwa kutoa rushwa hivyo kikao hicho kinapaswa kuwa na maamuzi na maadhimio yenye dira na taswira njema kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Saturday, March 25, 2017
SERIKALI YAWAONDOA HOFU WANACHAMA PPF KUFUATIA UAMUZI WA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake ya kufunga Mkutano wa 26 wa Wamachama na Wadau wa PPF kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha, (AICC), jijini humo Machi 24, 2017. Kauli mbiu ya Mkutano huo ilikuwa, “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii”.
Katika hotuba yake pamoja na mambo mengine, Waziri alisema"Naomba niwatoe hofu Wanachama wa PPF, kuhusu uamuzi wa Mfuko kuwekeza kwenye viwanda, kwani uamuzi huu ni sahihi kwa sasa, ikizingatiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda, lakini pia Serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, wa kujenga uchumi wa viwanda." Alitoa hakikisho Waziri Mhagama.

Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw.William Erio, akionyesha furaha yake kufuatia mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika mkutano huo ambapo alisema, jumla ya washiriki 800 walihudhuria mkutano huo na hivyo Mfuko umefanikiwa kukuza uelewa wa Wanachama na wananchi kwa ujumla juu ya uwekezaji katika viwanda ambao Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kuifanya ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5, (2016/17-2020/21 na pia kwa madhumuni ya kuongeza mapato yatokanayo na uwekezaji na kupanua wigo wa kuandikisha wanachama kutokana na ajira zitakazoongezeka.
Friday, March 24, 2017
MUWSA WAADHIMISHA WIKI YA MAJI KWA KUPANDA MITI KATIKA VYANZO VYA MAJI.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) John Ndetiko akiwa amebeba mti tayari kwa ajili ya kuotesha kando ya chanzo cha maji cha Shiri kilichopo wilayani Hai.
TIMU YA RIADHA YAKABIDHIWA BENDERA ,YAELEKEA UGANDA, KUREJEA NA MEDALI
Thursday, March 23, 2017
KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MRADI WA KINYEREZI
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo, (aliyesimama), akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea Mradi wa Umeme wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam, leo Machi 23, 2017
Meneja Msimamizi wa Mradi wa Kinyerezi I, Yuka Mukaibo kutoka kampuni inayojenga mradi huo ya Sumitomo kutoka Japan, akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati walipotembelea eneo la Mradi jijini Dar es Salaam, Machi 23, 2017. Wakwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Palangyo, na wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.NA K-VIS BLOG
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limeomba Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ishauri Mamlaka iruhusu mizigo yake iliyokaa bandarini kwa muda mrefu kutokana na swala la kodi iruhusiwe ili iweze kukamilisha Mradi wa ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa Kinyerezi.
Hayo yamesemwa na uongozi wa TANESCO wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyofanya kwenye Mradi huo jijini Dar es Salaam, Machi 23, 2017 ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo muhimu.
“Mashine na vifaa vilivyozuiwa bandarini viruhusiwe ili vikakamilishe mradi wa umeme wa Kinyerezi I&II na kodi zinazopaswa kulipia mashine hizo zilipwe baadaye ili kuruhusu kazi ya kufunga mitambo hiyo kwenye Mradi huo iweze kukamilika kwa wakati.” Alisema Meneja wa Mradi kutoka TANESCO akiiambia kamati hiyo
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, AIPONGEZA PPF KWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA

Mkutano Mkuu wa mwaka wa 26 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha, (AICC), leo Machi 23, 2017. Kauli mbiu ya mwaka huu ya mkutano huo ni, “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii”

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (pichani juu), ameupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kutekeleza kwa vitendo Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda..
Waziri ametoa pongezi hizo leo Machi 23, 2017 wakati akifungua Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwenye ukumbi wa Simba wa KItuo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
“Nimeelezwa kuwa nyinyi PPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Jeshi la Magereza mmeingia kwenye makubaliano ya pamoja ya kuanzisha viwanda vikubwa na vya kisasa vya kuzalisha sukari katika eneo la Mkulazi na Mbigiri Morogoro.” Alisema Waziri Dkt. Mpango
Monday, March 20, 2017
TANGA UWASA YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI
Mtaalamu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Ramadhani Nyambuka akisistiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma kwa mteja wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji Machi 22 mwaka huu
BI. KAGANDA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Bi.Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, mmoja wa wagombea ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki akikabidhiwa fomu na Bw. Said Bakari wa Idara ya Uhusiano wa kimataifa katika makao makuu ya CCM mtaa wa Lumbumba jijini Dar es salaam.
Bi. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, mmoja wa wagombea ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki akitoka nje baada ya kukabidhiwa fomu za kugombea nafasi hiyo makao makuu ya CCM mtaa wa Lumbumba jijini Dar es salaam. Bi Kaganda alifika hapo akiwa peke yake na bila mbwembwe akiwa na imani kwamba dhamira yake ya kusimamia na kutetea maslahi ya kina mama na watoto katika jamii ni agenda yake itayomsimamia katika kinyang'anyiro hicho.
SOKO LA MBAO LIMESHUKA WILAYANI MUFINDI
Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akiongea na wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi juu ya malamiko yao kwa TRA mkoa wa IringaNa Fredy Mgunda,Mufindi
Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi wamesema kuwa soko la mbao limeshuka kwa kiwango kikubwa kutoka na mrundikano wa kodi katika wilaya hiyo tofauti na wilaya nyingime. “Ukienda mbeya,njombe na maeneo mengine kodi ya vibali ni ndogo kuliko ya hapa mufindi sasa tunataka kujua tatizo nini”walisema wafanyabiashara
Aidha wafanyabiasha hao wameiomba mamlaka ya mapato mkoa wa iringa TRA kutoa kibali cha usafirishaji kwa kuondoa usumbufu wa tozo za ushuru check point na kuombwa lisiti za mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia mbao na nguzo.
Akizungumza mmoja wa wafanyabiashara hao Zakayo Kenyatta Katika mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu na TRA alisema kuwa TRA wamekuwa wasumbufu sana check point kwa kuwasimamisha zaidi ya siku tatu wakidai lisiti hizo huku wafanyabiashara wakionyesha barua za watendaji kutoka vijiji walivyonunulia zikikataliwa.
Saturday, March 18, 2017
MD KAYOMBO AWAONYA MAAFISA WATENDAJI WA KATA NA MITAA KUTOPOKEA RUSHWA
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa
ufafanuzi wa muongozo wa ukusanyaji wa mapato kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa
Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
MD Kayombo akisisitiza jambo
Friday, March 17, 2017
KIKOSI 841KJ MAFINGA KIMESHEREKEA MIAKA 50 KWA KUJENGA KIWANDA CHA NAFAKA

Mgeni rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa kutimiza miaka 50 pamoja na kuzindua jarida maalum la kikosi hicho akiwa amelishika linaitwa Uhodari.

Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha 841kj wakionyesha ukakamavu wake kwa kushindana kuvuta kamba ikiwa na lengo la kuburudisha wakati wa sherehe za miaka 50 ya kikosi cha 841kj
Na Fredy Mgunda,Mafinga
Kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga kimeanzisha kiwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha lengo likiwa ni kuhakikisha jeshi hilo linajilisha na kupata mahitaji mengine kupitia uzalishaji mali.
Akizungumza kaimu kamanda wa kikosi cha 841 kj mafinga Captain Victor Nkya katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 15 / 03 / 1967 kikiwa na lengo la kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kuwa na serikali ya viwanda kwa kuanza kujenga kiwanda cha nafaka na mifugo ambacho kitatoa ajira wa watu wengi na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla pamoja na kuimalisha ulinzi kutokana na majukumu waliyonayo.
Thursday, March 16, 2017
RAIS DKT MAGUFULI ATEMEBELEA ENEO LA UJENZI WA IKULU MPYA KIJIJINI CHAMWINO, DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wahandisi na maafisa wa Wakala wa Majengo ya Serikali wakati alipowasili kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
Sehemu ya matofali katika eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo wakati alipotembelea na kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
TANGA UWASA INAHITAJI BILIONI 15 KUTEKELEZA MPANGO WA KUSAFISHA MAJITAKA
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akizungumza jambo wakati wa kikao hicho leo
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka katika Jiji la Tanga (Tanga-Uwasa), linahitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 hadi 20 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kusafisha majitaka yaweze kutumika kwa shughulinyingine za kibinadamu ikiwemo kilimo cha umwagiliaji.
Akizungumza katika semina kwa wanahabari Jijini hapa Mkurugenzi wa Tanga-Uwasa Injinia Joshua Mgeyekwa, alisema kutokana na kuzaliza kiasi cha mita za ujazo zipatazo 2,700, wameonelea wayasafishe kwa kujenga mfumo utakaosaidia maji hayo kutumika tena.
Mgeyekwa alisema tayari wametenga eneo la Utofu kama sehemu itayokusanya maji taka ambayo kwa sasa kiasi cha asilimia 10 cha wateja wao maji wanayoyazalisha kupelekwa baharini hivyo mfumo huo utasaidia suala zima la uchafuzi wa mazingira.
Wednesday, March 15, 2017
DAWASCO KUTUMIA WIKI YA MAJI KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WAKAZI WA DSM
Na Mwandishi wetu.
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) limepanga kutumia maadhimisho ya 29 ya wiki ya maji inayoanza kesho kutoa elimu ,kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi kupitia Dawati maalumu katika vituo vyote 10 vya DAWASCO vilivyopo katika Jiji la Dar es salaam , Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Utaratibu huu umelenga kutoa mwanya kwa wananchi wanaopata huduma ya maji kutoka Dawasco ,kupata Elimu ya Huduma ya Maji na kusikilizwa kero na malalamiko yao ili kujenga ukaribu zaidi kati ya DAWASCO na wananchi.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Everlast Lyaro amesema madawati haya yatakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa wiki nzima ya maadhimisho haya ya wiki ya Maji.
Amesema zoezi la kupokea kero na malalamiko kwa waanchi litafanyika hadi siku za Jumamosi na Jumapili ambapo Madawati yatakuwa wazi ili kutoa nafasi zaidi kwa wananchi wengi kuwasilisha changamoto zao na kupatiwa utatuzi.
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) limepanga kutumia maadhimisho ya 29 ya wiki ya maji inayoanza kesho kutoa elimu ,kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi kupitia Dawati maalumu katika vituo vyote 10 vya DAWASCO vilivyopo katika Jiji la Dar es salaam , Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Everlast Lyaro amesema madawati haya yatakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa wiki nzima ya maadhimisho haya ya wiki ya Maji.
Amesema zoezi la kupokea kero na malalamiko kwa waanchi litafanyika hadi siku za Jumamosi na Jumapili ambapo Madawati yatakuwa wazi ili kutoa nafasi zaidi kwa wananchi wengi kuwasilisha changamoto zao na kupatiwa utatuzi.
POLISI KILIMANJARO YANASA SILAHA,DAWA ZA KULEVYA NA VIROBA VILIVYOPIGWA MARUFUKU
NITAHAKIKISHA SHULE ZOTE MAFINGA MJINI ZINAKUWA NA UBORA : COSATO CHUMI
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi madawti kwa viongozi wa kata ya sao hill kwa ajili ya matumizi ya shule
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipongezwa na viongozi wa kata ya sao hill kwa jitihada wanazozifanya kuleta maendeleo katika jimbo la mafinga mjiniNa Fredy Mgunda,Mafinga.
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ameendelea kutatua changamoto mbalimbali za jimbo hilo kwa kufanya ziara kwenye baadhi ya shuleza msingi zilizopo katika mjini wa mafinga na kukagua baadhi ya miundombinu inayoendelea kukarabatiwa kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wake.
Katika ziara hiyo Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo,mifungo 10 ya saruji,madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na Kinyanambo ambayo yalitolewa na wakala wa shamba la miti Sao Hill huku chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mafinga Mji kupitia mwenyekiti wake Yohanes Cosmas wakichangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za mbunge za kukamilisha ujenzi wa miundombinu hiyo.
Tuesday, March 14, 2017
JAMII YA WAFUGAJI NGORONGORO WATOA MALALAMIKO YAO KWA KAMATI YA BUNGE
Wananchi wa jamii ya wafugaji waliposimama katikati ya barabara ya kuingia Makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kwa lengo la kuzuia msafara wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii ilipotembelea Ngorongoro.
Wananchi wa jamii ya wafugaji wanaoishi katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro wakilelekea makao makuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro mara baada ya kuomba kutoa kero zao mbele ya kamati hiyo.
Monday, March 13, 2017
MAXCOM AFRICA (MAXMALIPO) INAWAKARIBISHA KUNUNUA HISA KWA NJIA YA MTANDAO
Kampuni ya Maxcom Africa (Maxmalipo) inawakaribisha watanzania kushiriki manunuzi ya hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye Soko la hisa la Dar es salaam(DSE) kwa njia ya mtandao (simu za kiganjani) na kufanya malipo kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo waliopo nchi nzima Tanzania.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu Bwana. Deogratius Lazari Mosha, Leo 13/03/2017 amewaambia waandishi wa habari kwamba Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na soko la hisa la Dar es Salaam(DSE) kwa kutumia mfumo madhubuti wa simu za viganjani unamwezesha Mtanzania kuweza kushiriki kwenye Manunuzi ya hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la awali la mitaji (primary markets ) kwa kupiga *150*36#, ameongeza kwamba baadhi ya makampuni hayo kwa sasa ni Vodacom na TCCIA.
Akifafanua hili Bw. Deogratius Lazari amesema ili Mtanzania aweze kushiriki Manunuzi ya hisa kwa mfumo huu anatakiwa kubonyeza *150*36# kisha ataingia kwenye Menyu ya soko la hisa na Kuchagua IPO kisha atachagua kampuni anayotaka kununua hisa, baada ya kufanya hivyo mteja atalazimika kujisajili na kisha atapata nafasi ya kuainisha idadi ya hisa anazohitaji(zisizo pungua 100 katika awamu ya kwanza).
Friday, March 10, 2017
Thursday, March 09, 2017
UTEKELEZAJI SERIKALI MTANDAO EP 01
Hiki ni kipindi cha Utekelezaji wa Serikali Mtandao nchini kinachotoa elimu kwa umma jinsi Serikali mtandao ilivyorahisisha utendaji kazi kwa Taasisi za Serikali na utoaji huduma kwa umma kupitia mtandao.
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA ENEO LENYE MGOGORO LA PORI TENGEFU LA LOLIONDO
Msafara wa Magari ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Malisili na Utaalii,yakpita katika maeneo mbalimbali ya Pori Tengefu la Loliono kwa ajili ya kujionea hai halisi ya mgogoro ulioo katika eneo hilo.
Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi ,Maliasii na Utalii,Atashasta Ndetiye (katikati) akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo kutizama vyanzo vya maji vilivyoko katika Pori Tengefu la Loliondo.
Subscribe to:
Comments (Atom)




