Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo,(wanne kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Afya), Dkt. Zainabu Chaula,(kulia), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Daniel Chongolo, (wapili kushoto), na viongozi wengine, wakiangalia kitanda cha kujifungulia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na PPF.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kushoto), Viongozi wa Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido, wakitembelea wodi ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Longido, ambapo ni moja kati ya vituo vilivyonufaika na msaada huo wa vifaa tiba kama sehemu ya mchango wa PPF kwenye Jamii.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PPF,
umekabidhi vifaa tiba katika Mkutano wake wa 26 wa Wanachama na Wadau.
Vifaa tiba hivyo vyenye jumla ya shilingi 99,983,700/- vilikabidhiwa kwa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa niaba
ya Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa PPF.
Msaada huo utatolewa katika hospitali na vituo vya afya 16 nchini kama mchango wa PPF kwa shughuli za kijamii.
Wakati
wa kufunga Mkutano huo, mgeni rasmi Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu
aliungana na Bodi ya Wadhamini wa PPF, Menejimenti na baadhi ya
Wafanyakazi wa PPF walienda kukabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha
Afya, Longido, ambacho ni moja kati ya vituo vya Afya 16 nchini
vitakavyonufaika na msaada wa vifaa hivyo.
Mhe. Jenista Mhagama,
alisema, PPF imefanya jambo zuri la kusaidia Jamii na kuunga mkono
juhudi za Serikali katika kuwapatia huduma bora za afya wananchi wake.
“Hivi
sasa akina mama wa Longido, mtajifungua katika mazingira mazuri nimeona
kati ya vifaa tiba vilivyotolewa leo ni pamoja na kitanda cha
kujifungulia hongereni sana PPF.” Alisema Mhe. Mhagama.
Akizungumza
kwenye hafla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William
Erio, alisema, msaada wa vifaa hivyo ni moja ya majukumu ya Mfuko
kusaidia jamii.(CSR), hivyo PPF itatoa msaada kama huo kwa hospitali na
vituo vya afya vingine 15.
Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni
pamoja na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula, Mkuu wa Mkoa
wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe.Daniel
Chongolo, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bw.Juma
Mhina.
Waziri Mhe. Mhagama akitoahotuba yake
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw. Ramadhan Khijjah, (aliyesimama), akitoahotuba yake
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, akitoa hotuba yake
Wakurugenzi wa PPF; Waliovaa suti kutoka kushoto, Mkurugenziwa Mifumo ya Kompyuta, Bw. Riobert Mtendamema, Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Martin Mmari, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw.Steven Alfred na Meneja Kiongozi, Uandikishaji wanachama na Elimu, Mbarouk Magawa
Mkuu wa Mkoawa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, akitoa hotuba yake
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kulia), akizungumza jambo na mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bi.Sara Barahomoka
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw. Aggrey Mlimuka, (katikati), Mjumbe wa Bodi Bi.Amelye Nyembe, (kushoto), na Mkurugebnzi Mtendaji wa Halmashauriya Wilaya ya Longido, Bw. Juma Mhina, wakiwa kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga wa PPF, Bi. Uphoo Swai, (katikati), akiwa na mwenyeji wa Longido wakifuatilia hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa PPF, Bw. Martin Mmari
Wakurugenzi na Mameneja wa PPF pamoja na watumishi wa Halmashauriya Wilaya ya Longido wakijumuika kwenye hafla hiyo
Wananchi wa Longido walikuwa ni mashahidi wakati wa kupokea msaada huo
Mkurugenzi Mkuu wa PPF naujumbe wake wakipokewa na viongozi wa Kituo cha Afya Lungido walipowasili kukabidhi msaada huo
No comments:
Post a Comment