Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akiongea na wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi juu ya malamiko yao kwa TRA mkoa wa Iringa
Na Fredy Mgunda,Mufindi
Wafanyabiashara wa mazao ya misitu
wilayani Mufindi wamesema kuwa soko la mbao limeshuka kwa kiwango
kikubwa kutoka na mrundikano wa kodi katika wilaya hiyo tofauti na
wilaya nyingime. “Ukienda mbeya,njombe na maeneo mengine kodi ya vibali
ni ndogo kuliko ya hapa mufindi sasa tunataka kujua tatizo nini”walisema
wafanyabiashara
Aidha wafanyabiasha hao wameiomba mamlaka ya
mapato mkoa wa iringa TRA kutoa kibali cha usafirishaji kwa kuondoa
usumbufu wa tozo za ushuru check point na kuombwa lisiti za mashine
kutoka kwa wakulima waliowauzia mbao na nguzo.
Akizungumza mmoja
wa wafanyabiashara hao Zakayo Kenyatta Katika mkutano wa wafanyabiashara
wa mazao ya misitu na TRA alisema kuwa TRA wamekuwa wasumbufu sana
check point kwa kuwasimamisha zaidi ya siku tatu wakidai lisiti hizo
huku wafanyabiashara wakionyesha barua za watendaji kutoka vijiji
walivyonunulia zikikataliwa.
"Tunawaomba TRA mkatoe elimu kwa
mkulima mmoja mmoja kwa sababu ni ngumu sana mkulima wa chini akuulizie
nguzo 5 alafu awe na lisiti ya mashine kwa hiyo tunawaomba TRA wakatoe
elimu hiyo na kuwaamasisha wakulima hawa Kuwa na hizo mashine kwani
wakulima hao ni wale ambao wanauza miti yako kutokana na matatizo mbali
mbali walionayo na sio kampuni" alisema Kenyatta
Akijibu hoja
hiyo meneja msaidizi WA TRA mkoa WA iringa Mustapha Mkilamwenye alisema
Kuwa wamekuwa wakiogopa kwenda kutoa elimu hizo kwa wakulima kutokana na
mkutano yao kuharibika kwa kuzomewa na kutokufikia muafaka WA
uelimishaji.
Pia Mkilamwenye amewataka wafanyabiashara hao kupata
kibari cha kununua na kusafirisha kutoka TRA wilaya au mkoa kabla
hqwqjaenda vijijini kununua ili kukwepa uwumbufu huo check point.
"Ombi
lenu tumelipokea hivyo tunawaomba kabla hamjanunua mpate kibali kutoka
TRA mkoa au wilayani kuokoa usumbufu WA tozo za ushuru check point, pia
tutatoa elimu ya matumizi ya mashine kwa wakulima vijijini wauzapo miti
yako kwa wafanyabiashara" alisema
Kwa upande wake Mbunge wa
mafinga mjini Cosato Chumi alisema Kuwa ameamua kuwakutanisha
wafanyabiashara na TRA kupata ufafanuzi WA kuombwa ushuru check point
kutokana na kulalamikiwa na wafanyabiashara hao Kuwa magari yako
wamekuwa wakikaa check point zaidi ya siku tatu wakiombwa lisiti za
mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia nguzo na mbao.
"Mkutano
huku ni mahususi kwa wrote tukipata ufafanuzi na kujua kwa nini
mnakamatwa check point na mkiobwa ushuru au njia kila mkoa,tra wanapaswa
Kuwa rafiki Wa wafanyabiashara na sio adui kwa sababu mufindi ndio
chanzo kikuu cha mapato ya nchi kutokana na zao LA mbao" alisema Chumi
Meneja
wa TRA wilayani ya Mufindi Filmoni Mwakapesile alisema Kuwa "ni kweli
tuhuma hizo na lawama tumezipata na tumekuwa tukipokea simu nyingi za
wafanyabiashara na kutatua matatizo yako lakini Leo tunashukuru Mbunge
amekututanisha na tumewapa uelewa na sisi kama TRA tumewaambia mini cha
kufanya kuondoa huo usumbufu"
Baadhi ya wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi waliohudhulia mkutano wa pamoja kati ya mbunge,TRA na wafanyabiashara.
No comments:
Post a Comment