Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo, (aliyesimama), akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea Mradi wa Umeme wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam, leo Machi 23, 2017
Meneja Msimamizi wa Mradi wa Kinyerezi I, Yuka Mukaibo kutoka kampuni inayojenga mradi huo ya Sumitomo kutoka Japan, akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati walipotembelea eneo la Mradi jijini Dar es Salaam, Machi 23, 2017. Wakwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Palangyo, na wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
NA K-VIS BLOG
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limeomba
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ishauri Mamlaka iruhusu mizigo yake
iliyokaa bandarini kwa muda mrefu kutokana na swala la kodi iruhusiwe
ili iweze kukamilisha Mradi wa ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa
Kinyerezi.
Hayo yamesemwa na uongozi wa TANESCO wakati wa
ziara ya Kamati hiyo iliyofanya kwenye Mradi huo jijini Dar es Salaam,
Machi 23, 2017 ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo muhimu.
“Mashine
na vifaa vilivyozuiwa bandarini viruhusiwe ili vikakamilishe mradi wa
umeme wa Kinyerezi I&II na kodi zinazopaswa kulipia mashine hizo
zilipwe baadaye ili kuruhusu kazi ya kufunga mitambo hiyo kwenye Mradi
huo iweze kukamilika kwa wakati.” Alisema Meneja wa Mradi kutoka TANESCO
akiiambia kamati hiyo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt.
Tito Mwinuka, naye aliongeza kwa kusema, “inatupa shida wakati
mwingine, wakati hela inatakiwa tulipe kule bandarini, uwezo wa TANESCO
katoka makusanyo sio mzuri sana kutokana na madeni, hivyo kama tungeweza
kuruhusiwa kutoa vifaa hivyo bandarini, ingekuwa vema kwani kasi ya
ukusanyaji mapato ya TANESCO inapoongezeka ndivyo tunavyoweza kulipa
lakini Mradi utakuwa umeendelea.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Mradi wa
Kinyerezi I&II utakapokamilika, utaweza kuzalisha umeme wa
Megawati 425, Naibu Mkurugenzi wa TANESCO, Mhandisi Khalid James
aliwaambia wajumbe wa Kamati hiyo. “Megawati hizi zitaunganishwa kwenye
Gridi ya Taifa na hivyo kuongeza umeme.” Alisema Mhandisi James.
Mradi
wa Kinyerezi I utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 188 huku
Mradi wa Kinyerezi II ukigharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni
344, aliongeza Mhandisi James.
Naibu Mkurugenzi wa TANESCO, Mhandisi Khalid James, (aliyesimama), akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa Mradi huo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini waliotembelea kujionea maendeleo ya Mradi huo
Meneja Mkazi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa Kinyerezi II, Markku Repo kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro(aliyenyoosha mkono), akifafanua mambo mbele ya wajumbe wa Kamati wakati wa ziara yao. Wakwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo.
Wajumbe wakitembelea Mradi huo huku wakiongozwa na Meneja Msimamizi wa Mradi, kutoka kampuni ya Japani ya Sumitomo
Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo, waksikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na wataalamu wa TANESCO na wajenzi wa mradi huo
No comments:
Post a Comment