Kama inavyotarajiwa na kutabiriwa na mashabiki wengi wa soka
nchini haswa mashabiki wa klabu ya Simba Wekundu wa Msimbazi, jijini Dar es
Salaam, ni kwamba mgombea katika nafasi
ya Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Michael Richard Wambura ameenguliwa katika
uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Akizungumza katika mkutano maaluum na waandishi wa habari
uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
jijini Dar es Salaam, Mweyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Simba Wakili Dr. Damas
Daniel Ndumbaru, amesema Wambura ameondolewa sababu kubwa mbili ya kwanza ikiwa
si mwanachama halili wa klabu hiyo.
Wambura alisimamishwa uanachama wa Klabu ya Simba tangu mei
5, 2010 kutokana na kosa la kuipeleka klabu hiyo mahakamani akifungua kesi
namba 100/2010 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyoko jijini Dar Es
Salaam.
Ndumbaru amesema kuwa Wambura aliwakilisha barua katika Kamati
ya Uchaguzi akikiri kuipeleka Simba mahakamani na kuiomba kamati hiyo kumaliza
swala lake na kuahidi kutorudia kosa kama hilo, jambo ambalo amepingana na
katiba ya klabu, TFF na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA).
Mwenyekiti huyo wa kamati amesema kuwa alipokea barua 2 toka
kwa Wambura ikiwa ni novemba 6, 2012 akitaka kujua uhalali wa uanachama wake na
nyingine septemba 15, 2012 ikijubu kuwa Simba haina tatizo lolote na yeye.
“Kuna utatata katika barua zake na pia kuna barua tatu
sept25,2012 ikieleza pia Simba hawana tatizo na Wambura” alisema Ndumbaru. Aliongeza
kuwa kutokana na kamati yake kujiridhidha na maelezo hayo imemuondoa Wambura
katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi june mwaka
huu.
Alieleza zaidi kutokana na maamuzi hayo Wambura hapaswi
kujishirikisha na shughuli za Simba kwa kifungu cha katiba no. 12 (3) ya mwka
2010 na ibara ya 12(3) 2014. Alieleza kuwa kama hatoridhika na maamuzi akate
rufaa kwenye kamati ya maadili ya TFF.
Amesema pia wengine wote waliowekewa pingamizi wamepitishwa
na wataendela na uchaguzi wa june 29 mwaka huu. Kwa kuondolewa Wambura nafasi hiyo imebaki na
watu wawili, Evans alieleeza Aveva na Andrew Peter Tupa, Makamu wa Raisi ni Jamhuri
Kiwelo Julio, Godfrey Nyange Kabour, Godfrey Itang’ale Kinesi na Swedi Nkwabi.
Wambua alipotafutwa alisema atazungunza kesho na waandishi,
na kwamba leo hayuko tayari kuongea na mtu moja moja.
No comments:
Post a Comment