Wednesday, April 09, 2014

TRA : EFDs HAZIJASITISHWA, ZINAENDELEA KAMA KAWAIDA

Serikali imekanusha taarifa za upotoshaji kuwa imesititisha matumizi ya mashine za Kielektroniki (EFD's) hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Julius Mjanga wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Akieleza Bw. Julius amesema taarifa kuwa matumizi ya mashine za kielektroniki yamesitishwa ni upotoshaji na hayana ukweli wowote.

(PICHANI: Kaimu Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Julius Mjanga akiwaeleza waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) kuhusu Taaarifa za Upotoshaji kuwa matumizi ya mashine za kielektroniki(EFD’s) yamesitishwa ila mashine hizo zinaendelea kutumika kwa mujibu wa Sheria na wafanyabiashara wanapaswa kuendelea kuzitumia il kuisaidia serikali katika ukusanyaji wa Kodi. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mkuu wa Mamlaka hiyo Bi Oliver Njunwa.)

Akifafanua zaidi Bw. Julius amesema kwa kuthibitisha kuwa taarifa hizo si za kweli kwani mnamo tarehe 26Februari 2014,Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda aliitisha kikao kati ya TRA,Wizara ya Fedha,Wizara ya Viwanda na biashara pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) .
Bw. Julius alibainisha kuwa katika kikao hicho Mh. Waziri Mkuu alielekeza kuwa orodha ya wafanyabiashara walioainishwa na kupewa barua iwekwe wazi kwa kubandikwa katika ofisi zote za TRA za Mikoa na Wilaya.
Pia Bw. Julius alisema kufuatia maelekezo hayo Mamlaka yaMapato Tanzania imeendelea kusimamia utekelezaji na usimamizi wa matumizi ya EFds unaoendelea na orodha ya wafanyabiashara husika ipo katika mbao za matangazo ya ofisi za TRA za Mikoa na Wilaya zote pamoja na kwenye tovuti.
Aliongeza kuwa TRA inatoa wito kwa wafanyabiashara wote nchini wenye sifa za kutumia mashine za kielektroniki ambao ni wa lengwa katika awamu ya pili kuzitumia kama sheria inavyotaka.
Bw. Julius aliwataka wananchi kutoa taarifa katika mamlka hiyo pale ambapo watatakiwa kutoa rushwa au kubugudhiwa wanapohitaji huduma katika ofisi za mamlaka hiyo kutoa taarifa katika vyombo vya dola au katika ofisi za TRA kupitia simu namba 0689122515 au ujumbe mfupi kwenye namba 0689122516.


No comments:

Post a Comment