Friday, April 11, 2014

MAPACHA WALIOUNGANA WANAABUDIWA INDIA, WAMEGOMA KUTENGANISHWA

Mapacha walioungana Shivantha na Shivram Sahu walishangaza wengi walipozaliwa nchini India, wakiwepo baadhi ambao ni waliwaabudu wakiamini kuwa ni mabadiliko ya kiungu. Na hata daktari mmoja aliposema inawezekana kuwatenganisha, watoto hao wenye umri wa miaka 12 waliozaliwa wameungana kuanzia kiunoni, wameamua kubakia pamoja.


Mapacha hao wanachangia miguu miwili na mikono mine na hushirikiana kufanya kazi sanjari. Inaaminika pia wanachangia tumbo lakini kila mmoja ana mapafu, moyo na ubongo wake. Mapacha hao wanaweza kushuka ngazi nyumbani kwao na hata kukimbia kwa kutumia viungo vyao sita(mikono na miguu) wanapokwenda kucheza mchezo wa kriket na michezo mingine na watoto wa majirani zao.

Na kwa mazoezi wamejifunza mambo mbali mbali ya nyumbani bila usumbufu wowote, ikiwa ni pamoja na kuoga, kula, kuvaa, na kuchanana nywele zao. Wana uwezo mkubwa katika masomo pia na kutambulika kuwa kati ya watoto wanaofanya vizuri sana shuleni kwao kitendo kinacho mfanya baba yao Raj Kumar, 45, mwenye watot wengine watano wa kike kujisikia fahari kubwa.

Madaktari wanaamini inawezekana kuwatenganisha mapacha hao, lakini matokeo yataporomosha uwezo wa Shivanath, ambaye anaonekana mnyonge kidogo kuliko mwenzie. Shivram yeye ndio atakuwa na fursa ya kubaki na miguu yote miwili na kuanza kuishi maisha ya kawaida wakati mwenzie hatakuwa na miguu na kuhitaji msaada wakati wote.

Kwa sababu hiyo mapacha hao na baba yao wanaona ni vyema wakabakia kuwa hivyo walivyo kuliko kutenganishwa. Baba yao aliiambia MailOnline:

‘Kwa kila mmoja ni jambo jema kuwaona wanangu, lakini mimi ndio naelewa shida na matatizo waliyonayo. Kipindi cha mvua ina kuwa ngumu kwao kutembea na mmoja anapotaka kukaa mwingine inabidi alale chini.

Lakini hawapigani. Wana mawazo sawa mmoja anapotaka kucheza mwingine anakubali. Mungu amewaumba namna hii kwa hiyo itabidi waishi kama walivyo. Sihitaji kitu kingine chochote. Hata kama madaktari wanasema, sintowatenganisha watoto wangu. Sina tamaa na hela. Ntafanya kazi kuwakuza. Sihitaji msaada.’

Shivram na aliongeza ‘hatutamani kutenganishwa. Tutabakia hivi hata tukizeeka. Tunataka kuishi kama tulivyo.’






No comments:

Post a Comment