Thursday, February 13, 2014

MUME AMNASA LIVE MCHUNGAJI AKIZINI NA MKEWE, AMPIGA PICHA

Mmoja wa vigogo na kiongozi wa kanisa la Seraphim Movement duniani, ambaye pia ni maarufu kama mtume I.T. Adewoye (Pichani) amehusishwa na tuhuma ya ngono hivi karibuni wakati ambapo mambo yanaendelea kumbadilikia katika taaluma yake ya uchungaji kutokana na kushindwa kuzui hisia zake.

Mchungaji huyo, ambaye pia ni maarufu kwa jina la Special Apostle/Prophet I.T. Adewoye ana umri wa miaka 70, ni kiongozi wa kiroho na mwanzilishi wa kanisa la Ayo Nio lililoko wilaya ya Idimu, Alimosho Lagos State Nigeria.




Kanisa hilo ni moja kati ya tawi matawi 53 nchini Nigeria, Marekani na Ulaya, ambapo kanisa la Ayo Nio ndio lenye waumini wengi kuliko yote. Imedaiwa kuwa Mtume Adewoye ana ushawishi mkubwa katika eneo hilo na huusishwa katika utatuzi wa migogoro mingi baina ya makundi na hata ya mtu mmoja mmoja.

Imedaiwa kuwa wanaokwenda kwake kwaajili ya kupata msaada wa kiroho katika jimbo la Lagos ni pamoja na Gavana wa jimbo hilo, Bw. Adejoke Orelope-Adefulire. Mtumishi Adewoye amekuwa na mahusiano ya mapenzi kisiri na Bi Balogun(Pichani Kushoto), muumini wa kanisa hilo na pia mke wa mtu.

SOMA ZAIDI...

Imeelezwa kuwa Adewoye amekuwa akifurahia mapenzi moto moto ya Bi. Balogun na kudaiwa wamekuwa wakifanyia katika kanisa hilo na wakati mwingine huenda hotelini.
Inadaiwa kuwa mara ya mwisho walikutana nyumbani kwa Bi Balogun ambapo pazia lilifunguliwa kidogo ili kuonesha kinachoendelea nyuma yake na kuonesha maisha ya mtu huyo wa Mungu.

Safari hii walikamatwa wazi kabisa na kupigwa picha na mume wa Bi. Balogun. Akiwa na hasira kali, Bw. Balogun alimkokota Mtume Adewoye polisi ambapo aliombwa kutomfungulia mashtaka.







No comments:

Post a Comment