Katika tukio la kutisha, wanajeshi wa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati kwanza walimchoma visu na kisha kumshushia mawe makubwa mtu aliyetuhumiwa kuwa ni mfuasi wa kundi la waislamu wa SELEKA. Kitendo hicho cha kutisha kimekuja muda mfupi baada ya sherehe za kuapishwa kwa Rais wa mpito Catherine Samba-Panza.
Bi Panza alihutubia majeshi hayo baada ya kuapishwa akidai umoja wa taifa hilo. Wapiganaji wa kundi la Seleka ambao wengi ni waislamu, walipindua serikali mjini Bangui mwaka jana. Mda mchache baada ya mapinduzi hayo nchi hiyo kwa miezi kadhaa sasa jeshi la nchi hiyo lilianza kutawanyika.
Mapigano baina ya waliokuwa wanajeshi wa Seleka na majeshi ya wakristo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na inakisiwa karibu robo ya wananchi wa taifa hilo wamekimbia fujo nchi hiyo
Mtu anayedaiwa kuwa ni Muislamu wa kundi la wapiganaji wa SELEKAakiwa amelazwa chini baada ya kupigwa na kuteswa na wanajeshi wa Jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati lililoko chini ya utawala wa mpito wa Raid Catherine Samba-Panza, tarehe 05/02/2014
TAHADHARI
PICHA ZIFUATAZO NI ZA TUKIO LA KWELI NA ZINAWEZA KUWAKWAZA BAADHI YA WASOMAJI WA HII BLOG, TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU HUU, TUNASHAURI PIA KAMA UNA ROHO NYEPESI TAFADHALI USIANGALIE.
Wanajeshi wakishirikiana na raia wakimburuta barabarani mtu aliyedaiwa kuwa ni mmoja wa wafuasi wa kundi la SELEKA huku wakimpiga mawe baada ya kumvua nguo mjini Bangui 05/02/2014.
CHINI: Mmoja wa wakazi wa Bangui akimrukia na kumtimba mtu anayesadikiwa kuwa ni mmoja wa wafuasi wa SELEKA kama anavyoonekana pichani.
Wanajeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakimtesa mmoja wa watu waliosadikiwa kuwa ni mmoja wa waasi wa Seleka, hivi karibuni mjini Bangui.
CHINI: Mmoja wa wanajeshi hao akirudishia kisu chake baada ya kumdhuru mtu aliyetuhumiwa kuwa alikuwa ni mfuasi wa kundi la SELEKA katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wanajeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakimtesa mmoja wa watu waliosadikiwa kuwa ni mmoja wa waasi wa Seleka, hivi karibuni mjini Bangui.
No comments:
Post a Comment