Sunday, February 16, 2014

DUNIANI KUNA MAMBO, AWEKEWA PUA KWENYE PAJI LA USO


Huyu jamaa mnaemuona kwenye picha hii ana miaka 22 ni mchina anaitwa Xiaolian. Xiaolian alipata ajali mbaya sana mwaka 2002 na kuahribu mfumo wa pua yake na kushindwa kupata matibabu ambayo yangeweza kumrudisha katika hali yake ya kawaida.

Matokeo yake yalisababisha Xialian kupata madhara makubwa kiasi cha kusababisha baadhi ya mishipa kuathirika na kushindikana kabisa kurudisha pua yake katika hali ya kawaida hata kwa upasuaji.



SOMA NA ANGALIA PICHA ZAIDI...

Hali hiyo ilisababisha wapasuaji kutafuta namna nyingine ya kumsaidia kwa kumtengenezea pua nyingine kwenye paji la uso wake ili kuachana na pua ya zamani.

Operesheni hiyo ilifanywa katika hospitali ya Fuzhou, Fujian, nchini China. Hii ilifanyika kwa kuvuta ngozi yake kwenye paji la uso na kisha kuweka tishu maalumu iliyokatwa kufanana na pua ambayo ilitolewa kwenye sehemu za mbavu za Xiaolian.

Wapasuaji wanasema pua hiyo mpya inaendlea vizuri na kwamba upasuaji zaidi utafanyika hivi karibuni.


No comments:

Post a Comment