Sunday, February 16, 2014

HATARI KUBWA: LACE WIG CHANZO CHA SARATANI

Baada ya kuchunguza saratani kwa miaka mingi imegundulika kuwa wanawake wengi hupatwa na saratani vichwani mwao kwasababu ya kuvaa lace wigi.

Utafiti umeonesha kuwa lace wigi inapovaliwa kwa muda mrefu zinatengeneza joto joto ambalo baadae huzalisha seli ambazo ni tofauti na zilizopo. Chanzo cha Lace wigi kupata umaarufu ni kuvaliwa sana na jamii ya wamarekani weusi, haswa vijana ambapo huiga wasanii na watu maarufu ili kufanana nao.

Uvaaji huo pia uliingia Afrika muda mrefu, Tanzania ni moja ya nchi ambazo lace wigi huvaliwa kwa kiasi kikubwa sana ambapo kuna msemo unaodaiwa kuwa “mwanamke nywele” ikimaanisha jinsi unavyokuwa na nywele nzuri ndivyo unavyoozidi kuvutia.


Kama kujichubua, wanawake wengi wameamua kubadilisha nywele zao pia na kutamani kufanana na wamarekani bila kujua madhara ya kufanya hivyo.


“Mi nafikiri kuna umuhimu wa kuzindua kampeni maalumu ya kupambana na hizi wigi” alisema mwakilishi wa taasisi ya saratani nchini Marekani Bw. Ronald DePinho alipoulizwa ni nini haswa kifanyike ili kuokoa maisha ya dada zetu katika janga la saratani.

“Kuna umuhimu pia wa kuingiza mistari kwenye nyimbo za hip hop mfano kama ‘kamata wigi tupa huko’ ili kuanza kusababisha jamii kuondokana nazo, hii ni kwasababu hao masuperstar ndio wanasababisha watu wengu kutamani kuzivaa” aliongeza mtaalamu mwingine Dr. Renald Depondo.



No comments:

Post a Comment