Saturday, January 04, 2014

MMH: WE SI UNASTAAJABU YA MUSA… SOMA HII HAPA

Siku ukitamani “ningekuwa na akili…” basi unaweza pata ubongo unauzwa kwenye mitandao.

Bw. David Charles, miaka 21, anadaiwa kudukua rekodi akitafuta vipimo mbalimbali, sio sababu anataka kuwa mtafiti bora, bali anatafuta namna atakavyo tengeneza fedha chapchap kwa kuuza viungo vya waliohifadhiwa katika makumbusho.
kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la TIME, Polisi wanadai Charles alikuwa anapekua rekodi za makumbusho (Indiana Medical History Museum), nchini Marekani kwa kufanya vipimo mbali mbali, ili auze viungo vya watu wa kale.
Charle anadaiwa kuiba ubongo wa mwanadamu na sehemu nyingine za viungo vya miili na kuiba vipimo toka kwa wagonjwa 2000 ambao mabaki yao yalihifadhiwa tokea mwaka 1890 mpaka 1940, kipindi hicho makumbusho hayo yakiwa ni hospitali.
Pamoja na upelelezi uliofanywa na polisi mwaka 2013 kuhusiana na upotevu wa vipimo hivyo bila mafanikio, polisi walipokea simu toka kwa mnunuzi mmoja kwa njia ya mtandao huko San Diego.
Kwa mujibu wa gazeti la Indianapolis Star, mnunuzi alisha nunua chupa sita za ubongo kutoka kwenye mtandao wa eBay kwa dola za kimarekani 600 (karibu sawa na shilingi 1,000,000 za kitanzania), pamoja usafirishaji dola 70, inasadikiwa ni kwa malengo maalumu.
Mnunuzi huyo alihisi ubongo huo unaibiwa baada ya kuona alama maalumu zilizowekwa kwenye chupa hizo, na ndipo alipoamua kupiga simu polisi na kufuatilia kwenye mtandao mpaka kumkamata muuzaji.
Baada ya kumwekea mtego, walimkamata na kumkuta anachupa 60 za viungo mbalimbali. Charles anashtakiwa kwa makosa mbalimbali likiwemo kukutwa na viungo vya binadamu, kukutwa na bangi, nk


No comments:

Post a Comment