Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika - PICHANI) Mwenye asili ya Asia ameshambuliwa na majabazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni )kwa kupigwa risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi mawili yaliyoojaa fedha.
Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo. Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG.
Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanya biashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.
PICHA NA HII TAARIFA ANGALIA HAPA...Jestina George
No comments:
Post a Comment