Sunday, January 05, 2014

ALIYEKUWA WAZIRI MKUU ISRAEL ANA NAFUU, HAJITAMBUI MWAKA WA 8 SASA


YUKO KITANDANI MWAKA WA 8 KWENYE KOMA



Madaktari wamefanikiwa kuirudisha hali ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Israel Ariel Sharon kuwa ya kawaida. Pamoja na jitihada hizo bado yuko katika hali mbaya, hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na msemaji wa hospitali.

Kwa mujibu wa CNN, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 85, ambaye amekuwa kwenye mashine kwa zaidi ya miaka 8, bado yuko hoi hospitali kutokana na baadhi ya viungo vyake kushindwa kufanya kazi, alisema Zeey Rotstein, ambaye ni Mkurugenzi wa Sheba Medical Center huko Tel Hashomer, Israel.


Sharon (Pichani) alichukua wadhifa wa Waziri Mkuu, Israel mwaka 2001. Lakini Sharon aligua na kupoteza fahamu(coma) toka mwaka 2006, alipopooza sehemu kubwa ya mwili wake na kulazimika kuwekwa kwenye mashine ya kupumilia. Kipindi chake kama Waziri Mkuu kilishaisha yeye akiwa hajitambui.

Iliripotiwa jumatano iliyopita kuwa hali yake imekuwa mbaya zaidi.


No comments:

Post a Comment