Sunday, January 05, 2014

ABIRIA 10 WADAIWA KUTUPWA BAHARINI LEO WAKITOKEA PEMBA

Imedaiwa kuwa abiria wapatao 10 wamerushwa baharini kutoka kwenye boti ya Kilimanjaro II waliyokuwa wakisafiria leo saa 5 asubuhi. Boti hiyo ya abiria ilikuwa ikitokea Pemba kuelekea Unguja, ndipo ilipokumbwa na dhoruba na watu hao kurushwa kwenye maji.

Boti hiyo ilipatwa na dhoruba ya upepo mkali katika eneo hatari la Nungwi. Walipohojiwa baadhi ya abiria katika boti hiyo walisema abiria hao ilibidi waachwe ili kunusuru usalama wa abiria wengine.

“Chombo kingeweza kuzama kama tungesema tusubiri waokolewe” alidai mmoja wa abiria huku akisisitiza asitajwe jina lake. Pamoja na kitendo cha kuondoka boti hiyo, abiria hao wakiwa kwenye maji walitupiwa maboya ili wajiokoe.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Zanzibar alidhibitisha kutokea kwa dhoruba hiyo na kusema “ni kweli boti ya Kilimanjaro II iliondoka Pemba kwenda Zanzibar saa mbili, ikiwa na abiria 369 ambao ni watu wazima na watoto 60, mabaharia 8”

Alieleza kuwa boti ilipofika kwenye eneo la hatari la Nungwi saa nne na robo ilipata dhoruba kutokana na upepo mkali.

Imedaiwa kuwa muda mchache baada ya tukio hilo baadhi ya abiria walichukua life jackets 5 na kuzirusha baharini bila maelekezo ya nahodha au amri toka kwa wafanyakazi wa boti hiyo.

Baada ya tukio hilo Boti hiyo ilenedelea na safari na kufanikiwa kufika salama Zanzibar muda wa saa 5.50. Hata hivyo polisi ilisema hakuna mtu aliyetumpwa na kuachwa majini kutokana na taarifa za nahodha wa boti hiyo aliyetambulika kwa jina moja la Aboubakar.





No comments:

Post a Comment