Thursday, December 05, 2013

MWANANCHI YAUNDIWA ZENGWE?

Wawekezaji katika tasnia ya Habari nchini Tanzania kutoka Kenya wameanza kupambana, huku kila mmoja akijaribu kushika soko la habari, Kampuni ya Nation Media Group ndiyo Kampuni pekee kutoka nchini Kenya iliyoweza kushika soko la habari kwa upande wa magazeti kwa muda mrefu.

Kampuni hiyo inayomilikiwa na Bilionea Aga Khan, ambaye ndiye mmiliki wa Hospitali za Aga Khan anayeishi nchini Ufanransa, huku Nation Media Group ikiwa chini ya utawala wa raia wa Kenya, ndiyo iliyokuwa Kampuni ya kwanza kumiliki chombo cha Habari Tanzania kwa mafanikio kupitia Gazeti la Mwananchi, Hata hivyo Kampuni hiyo imepata upinzani mkubwa kutoka kwa wakenya wenzao Kampuni ya The Standard, Nation ambayo kama ilivyo kwa Tanzania pia imekuwa ikiongoza tasnia hiyo nchini humo.
SOMA ZAIDI

Kampuni hiyo ilianza kuwa na migogoro ya uongozi mapema mwaka jana, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Mkenya Sam Sholei ambaye aliingia katika migogoro na Serikali ya Tanzania, baada ya serikali kukataa kumwongezea muda wa kukaa nchini kuliongoa Mwananchi, hata hivyo hatua hiyo ilimfanya Sholei kuondoka nchini na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazji Tanzania (TBC) Dunstan Tido Mhando, aliyefukuzwa kazi TBC na Rais Jakaya Kikwete.

Mbali na Sholei kuondoka nchini na kurudi nchini kwao Kenya, bado hali haikuweza kutulia ndani ya Nation Media Group, hatimaye akaondoka na kujiuunga na Kampuni nyingine ya Habari nchini humo The Standard, taarifa zinaeleza kwamba baada ya Sholei kuhamia The Standard alifanya mabadiliko makubwa kiasi cha kuifanya The Standard kuwa Kampuni imara nchini Kenya, huku Nation ikianza kujiendesha kwa hasara kila kukicha, hali kama hiyo pia ili ikumba Gazeti la Mwananchi Tanzania inayojiendesha kwa hasara kwa zaidi ya miaka miwili sasa.


Wakati Nation Kenya ikihaha kurudisha ubora wake baada ya wafanyakazi wengi kuondoka na kujiunga The Standard, nchini Tanzania hali imeanza kuwa tete baada ya The Standard kudaiwa kuinua Kampuni ya New Habari 2006, inayochapisha Magazeti ya Mtanzania,Rai The African,Bingwa na Dimba, hofu ya Mwananchi kuanguka ama kupotea kabisa katika soko la magazeti, imekuja katika kipindi ambacho gazeti hilo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu na Serikali ya Tanzania, wakati serikali ikidai kutekeleza sheria ya magazeti ya mwaka 1976 kwa kufungua magazeti na vyombo vingine vya Habari nchini.


Serikali imekuwa ikitekeleza sheria hiyo pale ambapo inabaini kwamba vyombo vya habari vinakwenda kinyume na sheria hiyo kwa jia ya machapisho yake, September 27 mwaka huu Serikali ilitumia sheria hiyo kulifungia Gazeti la Mwananchi kwa siku 14 huku Gazeti la Mtanzania likifungiwa kwa siku 90.


Hata hivyo Mwanchi ilisha maliza adhabu yake huku Mtanzania ikitarajia kumaliza adhabu hiyo December 25 mwaka huu,wakati wadau wa tasnia ya Habari nchini wakipinga sheria hiyo kwamba inakandamiza huru wa vyombo vya habari ,kutokana na uchakavu wake huku ikiwa na lengo la kuuwa vyombo vya habari,hali imezidi kuwa tete ndani ya Gazeti la Mwananchi kutokana na anguko linalolinyemelea.

Taarifa zilizonaswa na Habarimpya.com zinaelezwa kwamba anguko la Mwananchi nchini Tanzania pia imekuwa na mkono wa Serikali kutokana na kile kinachoelezwa kwamba ni hatua ya gazeti hilo kuwa sehemu ya Chama cha Upinzani ndani ya Serikali, hata hivyo taarifa kutoka ndani ya Kampuni hiyo zinaeleza kwamba mipango hiyo ilianza kusukwa mapema mwaka jana na tayari imekamilika, hatua hiyo inatokana na kundila kubwa la wafanyakazi wa Kampuni hiyo kuhamia katika Kampuni ya New Habari 206 kwa mshahara mnono.

Wanaotajwa kuhama ni pamoja na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi Denis Msaki pamoja na Chief Photographer Edwin Mjwahuzi,wakati kukiwa na kundi kubwa linalohama kwa upande wa waandishi katika idara ya matangazo na wasanifu kurasa za magazeti tayari wameshaanza kutumikia ajira zao mpya katika Kampuni hiyo, huku idadi ya watu 20 wakiwemo waandishi wa habari,madereva,watunza fedha,matangazo,usambazaji wakitarajia kuanza kazi rasmi January mosi mwaka 2014,wakati kundi la mwisho litatoka kiwandani baada ya mitambo ya kuchapisha magazeti kukamilika hapo mwezi wa sita mwaka 2014.

CHANZO http://www.habarimpya.com


No comments:

Post a Comment