Thursday, December 05, 2013

PAPA: NILIWAHI KUWA BAUNSA KWENYE BAR

Kama mtakatifu Peter atahitaji msaada kwenye geti la Pearly, basi mrithi wake Pope Francis(Pichani) anaweza kuwa msaada na kuifanya kazi hiyo vizuri tu.

Mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis aliwahi kuwa baunsa katika kumbi za starehe nchini Argentina, aliwaambia wakatoliki kanisani nje ya jiji la Rome, Italy mapema wiki hii.

Kwa mujibu wa CNN, Papa aliwahi pia kufanya kazi za usafi ikiwa ni pamoja na kufagia lakini pia kufanya majaribio ya kemikali katika mahabara, alisema Papa Francis katika ushuhuda wake wa ‘Papa wa watu’ lakini pia kama kiongozi wa jumuiya ya Jeswiti huko Argentina.

Kwa mujibu wa mwandishi wa vitabu, Christopher Lowney, Papa alikuwa akiamka saa 11:30 asubuhi kufua nguo za wahubiri.

Pamoja na hayo Papa hakutoa maelezo ya kina kuhusu kazi yake kama baunsa na kwamba vinahusianaje na kazi yake ya leo kama Papa Mtakatifu na mtumishi wa Kristu lakini pia mkuu wa Kanisa Katoliki duniani.

Badala yake, Papa aliliambia kundi kubwa lilihudhuria kanisani hapo kuhusu ‘kazi yake akifundisha fasihi na somo la saikolojia, vilimwezesha kurudi na kuingia kanisani’ liliripoti jarida la Catholic News Service



Inaonekana kuingia kanisani ndio msingi mkuu wa Papa Francis siku hizi, hayo ni kutokana na taarifa rasmi ya hivi karibuni ya maneno 50,000 kuhusu mazungumzo yake na wakatoliki bilioni 1.2 duniani kote.

No comments:

Post a Comment