Wednesday, December 18, 2013

FINALI ZA KIGOLI 2013, KUFANYIKA DECEMBER 21

Mashindano ya kumtafuta Kigoli wa Tanzania 2013, yanatarajiwa kufanyika Disemba 21, mwaka huu katika ukumbi wa Letasi Lounge, Victoria jijini Dar es Salam.

Awali fainali hizo zilipangwa kufanyika Desemba 8, mwaka huu lakini kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo ilisababisha kusogezwa mbele.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Manywele Intertaiment, ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo, Maimartha Jesse alisema ukumbi ulioandaliwa awali ulikuwa wa wazi hivyo mvua ilisababisha kuahirishwa.

SOMA ZAIDI...

Maimartha alisema mpaka sasa washiriki sita ndiyo watakao gombania zawadi ya gari lenye thamani ya sh. 8,500,000 kwa mshindi wa kwanza huku wa pili na wa watu wakipata ajira katika Kampuni ya Chicago General Traders & Real Estate.

Alisema mbali na zawadi hizo, washiriki wote walioshiriki wamepatiwa mafunzo ya kujitambua kama wanawake na jinsi ya kujiajiri, baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.

"Katika fainali hizo burudani mbalimbali zitakuwepo na watacheza nyimbo za kikwetu kwetu ikiwa ni za bendi mbalimbali pamoja na taarabu," alisema Maimartha.

Maimartha alisema burudani zitaporomoshwa na wasanii Barnaba, Amini, Ally Nipishe, bendi ya Sky Light pamoja na Malaika hivyo aliwaomba watu wajitokeze kwa wingi.

Aliwataja Vigoli watakaopanda jukwaani kuwa ni Neema Danford, Suzan Ndae, Mariam Ramadhani, Monalisa pamoja na Brigita Morice.

Naye kiongozi wa bendi ya Malaika, Christian Bella alisema kuwa amejiandaa vya kutosha na bendi yake kwa ajili ya kutoa burudani ya kutosha kwa watakaokuja kushuhudia Kigoli atakayeondoka na gari.

"Nimejiandaa vya kutosha kuburudisha hivyo watu wajitokeze katika fainali hizo, kwa wingi kwa ajili ya kushuhudia mambo mazuri," alisema Bella.









No comments:

Post a Comment