Wednesday, December 18, 2013

USALAMA: FACEBOOK WANAONA KILA KITU MPAKA ULICHOTAKA KUPOST

Uchunguzi umebainisha kuwa watumiaji wa mtandao wa kijamii Facebook hawawezi kuficha siri zozote wakati wakiwasiliana na ndugu au jamaa zao kwa kuwa kila wanachokiandika, kufikiria na kukifanya tayari kinajulikana.

Hali hiyo inahusishwa na udukuzi wa aina yake kwa kile ambacho kinaelezwa kwamba, inawanyima haki ya faragha watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa mtandao wa Times.com umebainisha kuwa, hayo ni matokeo hasi kwa watumiaji wa Facebook kutokana na ukweli kwamba kila unachokiandika katika ukurasa wako wa faragha (inbox) kinaonekana na kinarekodiwa hata kama utakifuta wakati huo huo.

Lakini tambua kuwa, hata kama ujaainisha yale ya moyoni yote (unayewasiliana naye faragha). Tambua kuwa Facebook huwa wanahifadhi taarifa zote Öhaijalishi umefuta awali au umeandika. Facebook inahifadhi yote ambayo unataka kuyafanya hata kama unawasiliana kwa njia ya video na zinachambuliwa zote (udukuaji),î ilieleza sehemu ya utafiti wa Times.com.

SOMA ZAIDI...



Wasomi waliotoboa siri hizo wakati wa utafiti huo uliopewa jina la Facebook Self-Censorship ni mwanafunzi ambaye anasomea Stashahada ya Uzamili Chuo cha Carnegie Mellon, Sauvik Das ambaye huwa anafanya kazi kwa msimu katika kitengo cha uhandisi Kampuni ya Facebook na Adam Kramer ambaye ni msimamizi wa data za Facebook.

Walisema, suala la kutambua taarifa za mtu ni rahisi ambapo ushahidi huo ulithibitika baada ya kugundulika tayari taarifa za watu milioni tano ambao wanatumia Facebook na lugha yao kuu ya mawasiliano ni Kiingereza zimerekodiwa.

Kwa mujibu wa Times.com, Facebook wanadukua taarifa za watu wakati wa mawasiliano ya faragha kupitia ujumbe wa maneno, video (mnachozungumza), unachokiandika katika ukurasa wako wa nje (status updates), unapoandika taarifa katika ukurasa wa mtu au kutoa maoni sehemu yoyote.

"Haijalishi kama, haujaandika au umeandika unapofungua tu, ukurasa wa Facebook tayari taarifa zako zinakuwa wazi kwao, kupitia mfumo maalumu wa ukusanyaji data (metadata). Bila kujali ni taarifa za aina gani iwe mahusiano yako, Facebook hawajali, wanachotaka kujua ni kuhusiana na mambo unayotaka kuyafanya," iliongeza sehemu ya taarifa hiyo ya Times.com.

Utafiti huo unamaanisha kuwa, kama Kampuni ya Facebook kutoka nchini Marekani ambayo ilianza kufanya kazi rasmi mwaka 2004 kwa ajili ya kuwaunganisha watu wote duniani kwa njia ya mawasiliano ya kimtandao ili kuwa kitu kimoja inadukua taarifa za watu itakuwa inaumiza watu zaidi ya bilioni moja.

Pia utafiti huu unakuja wakati ambapo Marekani imeingia katika mgogoro na mataifa mengine juu ya kudukua mawasiliano ya simu za watu baada ya kufichuliwa na Edward Snowden ambapo alidai lengo lao ni kutafuta taarifa za kijasusi.

Snowden ambaye yupo mafichoni nchini Urusi, Ikulu ya White House nchini Marekani imepuuza pendekezo la kumsamehe ili akome kufichua taarifa zaidi.

Wakati huo huo Jaji wa Mahakama moja katika jimbo moja nchini Marekani amesema kuwa mtindo wa Shirika la Ujasusi la Marekani kukusanya data za kwenye simu za watu binafsi ni kinyume na katiba ya nchi.

Jaji Richard Leon alisema kuwa, tabia hiyo inaingilia taarifa za faragha za watu na kuwa haistahili na pia Wamarekani hawaishi kwa amani kwani simu zao zote zinadukuliwa.

Mmoja wa watu waliolishitaki shirika hilo kwa kufanya udukuzi wa simu za mkononi za watu na kukusanya data nyingi ya watu binafsi, Lary Klayman, alisema kuwa, shirika hilo sharti lijue kuwa linakwenda kinyume na sheria.

Klayman alilieleza Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa, baada ya Jaji Richard Leon kuamua udukuzi wa simu unaofanywa na Shirika la Ujasusi la Marekani unakiuka katiba ya nchi kuhusiana na kukusanya taarifa kwa njia isiyofaa alipuuzwa.

Baadhi ya taarifa ambazo hukusanywa na shirika hilo ni namba za simu za watu, nyakati walizopiga simu na tarehe walizopiga simu zao.

Jaji Leon alitoa agizo la muda la kuzuia shirika hilo kuendeleza udukuzi ingawa anasuburi serikali kukata rufaa.

No comments:

Post a Comment