Thursday, December 05, 2013

CHANZO CHA KIFO CHA PAUL WALKER CHATAJWA

Waandalizi wa maiti nchini Marekani kutoka ofisi ya Los Angeles County Coroner, wametolea ripoti kuhusuna na chanzo cha kifo cha mcheza sinema Paul Walker na Roger Rodas kilichosababishwa na ajali mbaya hivi karibuni.

Paul Walker aliyepata umaarufu mkubwa kutokana na mfululizo wa filamu za Fast and Furious wa nchini Marekani aliyekumbwa na mauti hivi karibuni kutokana na ajali ya gari na kusababisha mshtuko mkubwa uliopelekea mauti.


Marehemu Paul Walker wakati wa uhai wake (wapili kushoto) akiwa na washiriki wenzie wa filamu ya Fast and Furious, kutoka kushoto ni Dywne Johnson, Vin Diesal na Tyrese Gibson 
Paul Walker alifariki kutokana na majeraha mbalimbali aliyoyapata kutokana na ajali mbaya aliyopata novemba 30, 2013, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa.

Kwa mujibu wa mtandao wa BOSSIP, maelezo ya ripoti hiyo iliyotolewa na ofisi ya L.A County Coroner, ilitafsiriwa kuwa hakufa kwa mshtuko wa ajali hiyo pekee. Aliungua moto mpaka mauti yake baada ya gari aliyokuwemo aina ya Porsche GT kugonga mti na nguzo na hatimaye kulipuka na kuwaka moto.

Aliyekuwa anaendesha gari hilo la kifahari, Roger Rodas, alifariki pia kwa maumivu makali yaliyotokana na majeraha yaliyosababishwa na ajali hiyo. Inadaiwa kuungua haikutajwa kama chanzo cha kifo chake.

Ripoti ya wahudumia maiti hao ilidai, hewa yenye sumu kali ndiyo ilikuwa chanzo cha kifo cha watu hao wawili, na kwamba ripoti kamili itatolewa kati ya wiki 6 mpaka 8 zijazo.

Ripoti ya madaktari imeeleza kuwa chanzo cha kifo cha Walker na Rodas ni ajali. Ripoti ya ofisi ya Corona ilieleza kuwa wote wawili walitambulika kwa kutumia mfumo wa meno yao mdomoni.

Walker na Rodas walifariki jumamosi huko Santa Clarita, CA baada ya gari waliyokuwemo aina ya Porsche GT kuacha njia na kuvamia nguzo na mti na kisha kulipuka na kusababisha moto mkubwa.

Chanzo na sababu ya ajali hiyo bado vinachunguzwa. Paul alikuwa na miaka 40. Rodas miaka 38.

No comments:

Post a Comment