Friday, December 06, 2013

BREAKING NEWS: MANDELA AMEFARIKI

1 9 1 8 - 2 0 1 3

JOHANNESBURG – Nelson Mandela (95), Rais wa kwanza mweusi na alama ya kudumu ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, amefariki dunia jana (alhamisi). Mandela amefariki akiwa nyumbani kwake na familia yake

Serikali ya Afrika ya Kusini imetangaza taarifa hizo ambapo viongozi na taifa zima la Afrika Kusini limekumbwa na majonzi makubwa.

“Taifa letu limempoteza mtoto wa muhimu sana” alisema Rais Jacob Zuma jana usiku na kurushwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari.

Bwana Zuma aliongeza kuwa Bwana Mandela amefariki saa 2:50 jioni kwa saa za Afrika Kusini (sawa na saa 3:50 Tanzania)

“mapambano yake ya uhuru bila kuchoka yamempa heshima kubwa ulimwenguni. Uvumilivu wake, utu wake na huruma zake vimemfanya apendwe duniani”

Bw. Zuma alitaja kifo cha Bw. Mandela “kipindi cha huzuni kubwa kwetu” na kusema Afrika Kusini inaungania na familia ya raisi huyo wa zamani” wamejitolea sana na kuvumilia mengi ili watu wetu wawe huru” alisema Bw. Zuma

No comments:

Post a Comment