Kijana wa miaka 22 amepoteza maisha baada ya kutandikwa risasi 20 na polisi wakifikiri ameshikilia bunduki kumbe ni simu yake ya iphone.
Stephen Clarke (Pichani) alipoteza maisha akiwa uwani kwa bibi yake
Sacramento, Marekani usiku wa jumapili machi 18. Polisi wanasema waliona Clarke
ameshikilia kitu kama bunduki kabla ya kumfatulia risasi 20 na kupoteza maisha.
Polisi hao wawili walifika eneo la tukio kufuatia wito wa simu
ya 911 kuhusiana na tuhuma za uvunjaji dirisha la gari. Ndipo walipokutana na
Clarke na kuamini kuwa ndiye aliyekuwa anavunja dirisha hilo. Pia walimuona
ameshika kitu mkononi ndipo kila mmoja alimfyatulia risasi mara kadhaa ili
kumdhibiti.
Kijana huyo baba wa watoto wawili pia alikuwa anajiandaa
kufunga pingu za maisha alipoteza maisha papo hapo “alikuwa sehemu mbaya wakati
mbaya, nyumbani kwake? Hawakupaswa kufanya hivyo” bibi yake, Sequita Thompson
aliiambia Sacramento Bee.
“niliwaambia Polisi kuwa nyinyi ni wauaji” kilimuonesha
kipande cha video bibi huyo akibubujikwa machozi, ‘mmemtenganisha na watoto
wake” alisema
kwa mujibu wa shirka la Associated Press (AP), familia ya
Clarke imeeleza kuwa marehemu ameacha watoto wawili wakiume Cairo na Aiden
pamoja na mke mtarajiwa Salena Manni. Askari waliofanya tukio hilo
wamesimamishwa kazi wakati uchunguzi unaendelea
No comments:
Post a Comment