Na Mwandishi Wa Kimataifa
Immamatukio
Kiongozi wa dini Israel (chief rabbi) amezua mzozo kwa
kuwaita watu weusi “nyani’ wakati akiendesha ibada ya wiki. katika ibada hiyo,
Rabbi Yitzhaj Yosef alitoa matamshi ya dharau kwa lugha ya kiyahudi na kuwaita
watu weusi kuwa ni “nyani”
Matamshi hayo yalitafsiriwa kuwa yanaamsha “hisia za ubaguzi
wa rangi” jambo ambalo halikubaliki kwa wanaharakati kutoka maeneo mbalimbali
duniani.
Hata hivyo ofisi ya Rabbi Yosef ilijibu madai hayo kwa kudai
alinukuu maandishi kutoka katika kitabu cha Talmud ambacho ni kitabu cha sharia
ya Wayahudi. Yosef aliwahi kuleta mzozo baada ya kusema wanawake wa kidunia
wanatabia za kinyama sababu wanavaa nguo za kuaibisha.
Rabbi ni kiongozi wa jamii ya Wayahudi wa Sephardic waliloko
Mashariki ya Kati pamoja na wale wa kaskazini mwa bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment