Mbunge wa CCM Samwel John Sitta (PICHANI JUU) ameshinda Kura 487 na ndiye mshindi na anakuwa Mwenyekiti mpya wa Bunge la Katiba.Hashim Rungwe Kura 69, zilizoharibika 7.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki,Mh Samwel Sitta ameibuka kinara kwenye nafasi aliyowania ya kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba mara baada kumbwaga mpinzani wake.
Wakili wa Kujitengemea Ndugu Hashim Rungwe,Sitta anaibuka kinara na kuichukua nafasi hiyo ya kuwa Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo Maalum la Katiba kufuatia Mwenyekiti wake wa Muda,Mh Ameir Pandu Kificho,ambaye mda wake wa kuliendesha bunge hilo unakoma leo.
Jumla ya Kura zilizopigwa ni 563 na zilizoharibika ni 7,kufuatia idadi hiyo ya Kura Ndugu Hashim Rungwe amepata kura 69 na Mh.Samwel Sitta ameibuka na kura 487,kwa Matokeo hayo imetangazwa kuwa Mh.Samwel Sitta ndiyo mshindi.

No comments:
Post a Comment