Monday, February 15, 2016

SIKU CHACHE KABLA YA UCHAGUZI UGANDA, DR. BESIGYE AKAMATWA

Na Mwandishi Wetu,

Ikiwa ni siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Uganda kufanyika, mgombea wa Uraisi kutoka champ cha upinzani cha FDC na mwenye ushawishi  mkubwa nchini humo, Dr. Kizza Besigye amekamatwa na polisi jijini Kampala ambapo ni mji mkuu wan chi hiyo.

Kwa mujibu wa BBC NEWS, shuhuda alioona tukio hilo anasema, polisi walitumia mabomu ya machozi kutawanya kundi la mamia ya waandamanaji wakati tukio hilo likiendelea.


Besigye ni mmoja kati ya wagombea saba wa upinzani wanao wania kumng’oa Rais Yoweri Musseven ambaye ameongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 30 katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika siku ya jumatano.


No comments:

Post a Comment