PICHANI : Rais wa Marekani, Donald Trump akiwa amezungukwa na wafanyabiashara pamoja na maafisa wa wa nchi hiyo, akijiandaa kutia saini taarifa itakayopitisha mpango wa kutoza faini bidhaa za China, katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Washington, Marekani. (Reuters)
Na Mwandishi Wetu wa Kimataifa,
Immamatukio Blog.
China imeitaka Marekani kuachana na malengo yake wakati Rais Trump akiandaa mpango wa kutoza ushuru mpaka kufikia dola bilioni 60 (sawa na shilingi trilioni 135.5 za Tanzania) bidhaa za China, jambo ambalo linaonesha dalili ya vita ya biashara baina ya mataifa hayo makubwa kiuchumi duniani.
Kwa mujibu wa taarifa ya Rauters, kuongezeka kwa mvutano baina ya Beijing na Washington kumeleta wasiwasi katika masoko ya fedha ambapo wawekezaji wanabashiri matokeo mabaya ya kiuchumi duniani kama patatokea vikwazo vya kibiashara.
Trump anapanga kutoza kodi katika kile utawala wake unachokiita kukosekana kwa usawa katika hatimiliki za Marekani. Uchunguzi ulianza mwaka jana chini ya kifungu 301 cha mwaka 1974 cha Sheria ya Biashara ya Marekani.
“China haitarajii kuingia katika vita ya biashara, lakini haiogopi kupambana” taarifa ya Wizara ya Biashara China ilijibu. China inatumaini Marekani itajitoa katika hatua hiyo na kufanya uamuzi sahihi ili kuondoa hatari za uhusiano”
Katika taarifa iliyosainiwa na Rais Trump jana(alhamisi), kutakuwa na majadiliano ya kipindi cha siku 30 ambayo yataanza baada ya orodha ya bidhaa za China kukamilika na kuchapishwa. Kipindi hicho kinatoa nafasi ya uwezekano wa maongezi kufanyika ili kufanyia kazi tuhuma za Trump kuhusu wizi wa hati miliki na kusababisha uhamaji wa teknolojia.
Japo ikulu ya White House imedai kuwa mpango wa ushuru huo ni matoke ya “uchokozi wa kiuchumi wa China”, Trump amesema anaichukulia China kama “rafiki” na pande zote ziko katika kipindi cha majadiliano. Nayo taarifa ya Wizara ya Biashara China imedhibitisha kuwepo kwa mawasiliano mazuri kwa pande zote.
Wakati hayo yakiendelea China imeonesha utayari wa mapambano kwa kuweka mkakati wa kutoza kodi ya dola billion 3 (sawa na shilingi tilioni 6.7 za Tanzania) dhidi ya bidhaa za matunda, mvinyo na karanga katika kujibu mpango Trump alioutangaza mapema mwezi huu katika chuma na aluminium, jambo ambalo utekelezajiwa unatakiwa kuanza ijumaa.
Vita hiyo ikitokea italeta athari kubwa kwa chumi zote zinazo peleka bidhaa zake nchi za Marekani na China.
No comments:
Post a Comment