Dar es Saalam
Imeelezwa kuwa, mbali ya kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya kuifanya Tanzania kuwa na umeme wa kutosha ifikapo mwaka 2025, Serikali pia imeazimia kufikia malengo ya Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Nishati Endelevu kwa Wote (SE4 ALL) ifikapo mwaka 2030.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati na Madini katika vikao baina yake na wawekezaji wa Kampuni mbalimbali katika sekta ya Nishati vilivyoanza tarehe 15- 18 Februari, 2016, kwa lengo la kujadili namna kampuni hizo zinavyoweza kufanya kazi na Tanzania hususan katika kuzalisha umeme ili kuweza kufikia malengo tarajiwa ya Taifa kuwa na umeme mwingi, nafuu na wa uhakika.
“Mpango wa SE4 ALL unalenga katika upatikanaji umeme kwa wote ifikapo mwaka 2030, ongezeko maradufu la utumiaji wa nishati jadidifu na matumizi bora. Rasilimali za kufikia huko tunazo na hivyo tunahitaji wawekezaji makini,”alisisitiza Profesa Muhongo.

Prof. Muhongo amesema Tanzania inahitaji kufikia malengo hayo yote, hali ambayo imefanya Wizara kuongeza jitihada za kuhakikisha inakutana na wawekezaji mbalimbali ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta hiyo ili kuweza kuhoji na kubaini kampuni ambazo zina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha ili kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Aliongeza kuwa, japokuwa Taifa lina uhitaji mkubwa wa nishati hiyo, lakini suala la kumpata mwekezaji makini, mwenye uwezo kiteknolojia, kifedha na uzoefu wa kutosha ni jambo ambalo Serikali inalichukulia kwa uzito mkubwa ili kufikia malengo tarajiwa.
Ameongeza kuwa, Serikali imelenga katika kuhakikisha kwamba, nishati inasaidia kuwezesha ukuaji wa uchumi, kuondoa umaskini na kuongeza pato la taifa kwa miongo kadhaa na hivyo kutumia fursa hiyo kuwakaribisha wawezekaji kupitia vyanzo mbalimbali vya nishati vinavyopatikana nchini, ikiwemo makaa ya mawe, gesi asilia, jotoardhi, upepo, jua na nishati nyingine.
Akizungumzia kuhusu nishati ya makaa ya mawe amesema ni wakati sasa wa Serikali kuongeza nguvu zaidi ili makaa hayo yaweze kuzalisha umeme nchini, ikizingatiwa kwamba, Taifa linayo akiba ya kutosha ya makaa hayo nchini.
“Kama Taifa tunataka kuweka nguvu kubwa katika rasilimali ya makaa ya mawe, si jambo zuri hata kidogo kutokuzalisha hata megawati moja ya makaa ya mawe wakati rasilimali za kutosha zipo. Ikiwa tunahitaji umeme nafuu na wa uhakika, makaa ya mawe yatakuwa na mchango mkubwa katika hili.
Aidha, alitumia fursa hiyo kuzitaka kampuni ambazo ziko katika hatua za kukamilisha taratibu zinazotakiwa hususani zile zinazolenga kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe, kuongeza kasi ya utendaji ili kuhakikisha kwamba, suala hilo halichukui muda mrefu.
Miongoni mwa Kampuni ambazo zimeonesha nia ya kuwekeza katika kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe ni Kampuni ya Ednville Energy plc, ambayo tayari imefanya utafiti katika maeneo ya Mkomolo na Namwele, mkoani Rukwa , ambapo kampuni hiyo imelenga kuzalisha megawati 300 kwa kutumia makaa ya mawe, na uwezo wa kuendelea kuzalisha kwa kutumia makaa hayo kwa kipindi cha miaka 35 kutokana na rasilimali iliyopo maeneo hayo.
Tanzania inatajwa kuwa tayari imetia saini Mpango wa Umoja wa Mataifa ya Nishati Endelevu kwa Wote (SE4ALL) ifikapo mwaka 2030, ambao utaiwezesha kufaidika na fedha zitakazotolewa ili kuendeleza miradi ya nishati. Aidha, bado iko katika nafasi nzuri ya kufaidika na mpango huo wa SE4 ALL, pia ndio nchi iliyoiwakilisha Afrika katika maandalizi ya mpango huo.
Profesa Muhongo ameanza kukutana na wawekezaji mbalimbali katika Sekta ya Nishati ikiwa ni jitihada za Serikali kufanya kazi na wawekezaji wa ndani na nje katika sekta hiyo ili kuwezesha ongezeko la nishati hiyo nchini.

No comments:
Post a Comment