Tuesday, February 16, 2016

BREAKING NEWS: WAZIRI AMFUKUZA KAZI MKURUGENZI WA BODI YA MIKOPO


Na MAELEZO

WaziriwaElimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Prof.Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa ajira wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, George Nyatega pamoja nakuwasimamisha kazi Wakurugenziwatatu.

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu matatizo ya kiutendaji na matumizi mabaya ya fedhazaUmmayanayofanyikaBodiyaMikopo.

Prof.Joyce Ndalichako amesema kuwa Taasisi ya Bodi ya Mikopo imeonesha utendaji usioridhisha kiasi kwamba kumekuwa na matatizo mengina yanayojirudiarudia kwa wateja wao mara kwa mara.

“Mikopo kwa wanafunzi imekuwa ikichelewa kuwafikia bila sababu za msingi kiasi kwamba imejengeka taswira kwa wanafunzi kwamba hadi walalamike wizara ni ndipo matatizo yao yashughulikiwe hivyo, tatizo sio ukosefu wa fedha bali ni uzembe wa watendaji katika kuwapatia wanafunzi mikopo yao kwa wakati.”Alisema Ndalichako.
Amewataja watumishi aliowasimamisha kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusuph Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaj iMikopo Juma Chagonja pamoja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo Onesmo Laizer.

Aidha,amezitaja baadhi ya sababu zilizosababishwa kufukuzwa na kusimamishwa kazi kwa watumishi hao zikiwemo za kufanya malipo yasiyo sahihi kwa baadhi ya wanafunzi wanaosoma ndani na nje ya nchi pamoja udhaifu uliobaini kakatika mifuko ya fedha.

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inajukumu la kutoa mikopo kwaajili ya wanafunzi wa elimu ya juu na kusimamia urejeshaji wa mikopo hiyo, kwa mwaka wa masomo 2015/2016 jumla ya Shillingi Bilioni 459 imetolewa mikopo kwa wanafunzi 122,486 wanaosoma katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment