Friday, January 29, 2016

RAIS MAGUFULI ATEUA MAKATIBU TAWALA WAWILI KWA MIKOA YA MWANZA NA KATAVI

RAIS Dkt.John Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu tawala wawili kwa Mikoa ya Mwanza na Katavi kwa lengo la kujaza nafasi za Makatabu tawala wa mikoa hiyo kwamujibnu wa Tarrifa ya Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue.

Akitangaza mabadiliko hayo Dar es Salaam jana Balozi Ombeni sefue alisema kuwa Rais ammteua Kamishina wa Polisi Clodwing Mtweve (Pichani chini) kuwa katibu tawala wa mkoa wa mwanza ambapo anakwenda kujaza nafasi iliachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitengeliwa.

Pia alisema kuwa kabla ya uteuzi huo Kamishna Mtweve alikuwa kamishna wa fedha na utawala wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Balozi Sefue alisema kuwa Rais Dkt.Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Paul Chagonja (Pichani juu Kushoto) kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Katavi ambapo anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Maden Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Pia alisema kuwa kabla ya uteuzi huo Kamishna Chagonja alikuwa kamishna wamafunzo na operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania na kuongeza Rais Magufuli amesema kuwa
ameamua kuwateua Makamishna hao wa Polisi kama alivyo wateua majenerali wa Jeshi la
wananchi Tanzania kuwa Makatibu wakuu wa Wizara,kwa lengo la kujenga nidhamu
katika utumishi wa umma.

Balozi Sefue alisema kuwa Makamishna Clodwing Mtweve na Paul Chagonja pamoja na
Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa balozi mpya wa Qwait wataapishwa
kesho juma mosi Januari 30 saa 4 asubuhi Ikulu Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment