Friday, January 29, 2016

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WASHIRIKI MKUTANO MKUU WA JUKWAA LA WAHARIRI MOROGORO

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha J. Mshomba(katikati waliosimama mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa Jukwaa La Wahariri, katika Hoteli ya Nashera, Morogoro (picha na Imma Matukio)

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Absalom Kibanda akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha J. Mshomba kutoa mada katika ukumbi wa Nashera Morogoro. WCF inakusudia kuanza kulipa mafao kuanzia julai mosi mwaka 2016. Kati ya mambo yaliyojumuisha mada hiyo ni pamoja na uchangiaji katika Mfuko, adhabu kwa mujibu wa sheria namba 20/2008. (picha na Imma Matukio)    

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha J. Mshomba akitoa mada kwa Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania wakiwa katika Mkutano Mkuu wa mwaka Mjini Morogoro leo tarehe 29.01.2016.(picha na Imma Matukio) 


Bw. Jesse Kwayu, Mhariri wa magazeti la kila siku ya The Guardian Limited akiuliza swali baada ya uwasilishwaji mada.    

Bi Hawla Shamte, Mhariri wa gazeti la Mwananchi akiuliza swali kuhusu mafao yatakayotolewa kwa wafanyakazi endapo wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.



Bw. Deo Mushi, Mhariri wa magazeti ya serikali (TSN) akiuliza swali baada ya uwasilishwaji mada.    

Bw. John Bwire, Mhariri wa magazeti ya Raia Tanzania akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) baada ya kuwakilisha mada mbele ya Wahariri wa vyombo mbalimbali nchini    

Bw. Paul Maregesi, Mhariri wa magazeti la kila siku ya New Habari akiuliza swali baada ya uwasilishwaji mada.    

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha J. Mshomba akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano mkuu wa Jukwaa la Wahariri unaoendelea mjini Morogoro.    






No comments:

Post a Comment