Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd na mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda natarajiwa kuwasili leo mchana saa 7 kamili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Navile Meena,
Kibanda atarejea leo kutoka Afrika Kusini, alipokwenda kutibiwa kutokana na kuvamiwa machi 5.
Kibanda alisafirishwa kwenda kutibiwa Afrka Kusini siku moja baada ya kuvamiwa na kupigwa nje ya geti la nyumbani kwake na watu wasiojulikana.
Taarifa hiyo iliyotumwa kwa wahariri imewataka waandishi pamoja na wahariri kukusanyika katika kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo saa sita ili kumpokea ambaye amekuwa nchni huko kwa miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment