Mkazi wa Dar es Salaam, Kawe eneo la bondeni karibu na
daraja akifanya biashara ya kuuza chenji ambapo chenji ya shilingi elfu moja unalipa shilingi 100. Mkazi
huyo sio tu anajukumu la biashara yake lakini pia ni mama mwenye mtoto ndogo. Wakati
picha hii inapigwa binti huyu alikuwa anamsumbua mama yake.
Taswira ya jiji la Dar es Salaam, hapa ni eneo la Tegeta
kama linavyoonekana. Hili nie eneo lenye shughuli nyingi kwa maisha ya kila
siku ya wakazi wa eneo hilo pamoja na maeneo ya Kunduchi, Wazo na hata Boko. Hapa
unaweza kuchanganyikiwa upite wapi kama eneo hilo linavyoonekana katika picha.
CHINI :Mpanda baskeli akiwa amebeba magunia ya mkaa akielekea
sokoni hivi karibuni, katika barabara mpya inayojengwa kutoka Msata mpaka
Bagamoyo. Sehemu kubwa ya barabara hiyo imeshakamilika na kubakiza kipande
kidogo chenye madaraja makubwa kadhaa likiwepo la mto Ruvu. Njia hii ndi
itakayotumika kwaajili ya mabasi yanayokwenda njia ya Tanga ikiwa ni pamoja na
Moshi Arusha.
No comments:
Post a Comment