Watafiti wamebaini kuwa mbu wanaobeba malaria huvutiwa
zaidi na harufu ya mwili kuliko wale wasio beba malaria. Imedaiwa kuwa mbu hao
hufuata harufu ya mwili wa binadamu zaidi kuliko wale wasio na malaria.
Utafiti uliofanywa na
Dk. James Logan umeonesha kuwa mbu
wanaobeba malaria hukimbilia haraka zaidi harufu ya mwili na wanauwezekano
mkubwa zaidi wa kuuma na hatimae kuambukiza malaria.
Malaria ni ugonjwa unaoambukiza kwa kuumwa na mbu na
kusababisha vifo vingi katika nchi mbalimbali duniani na kuathiri zaidi nchi
zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.
Utafiti unaonesha idadi ya vifo vya maleria
imeshuka kwa kiasi kikubwa duniani pamoja na kwamba maambukizi yamebaki kuwa ni
zaidi ya watu milioni 200 kila mwaka.
No comments:
Post a Comment