TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
1.
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) katika kikao
chake leo, Jumatano, Mei 15, 2013 limemsimamisha uanachama kwa muda
usiojulikana, Mhariri wa Mtanzania Jumatano, Charles Mulinda. Kwa maana hiyo
Mulinda ataendelea kuwa nje ya TEF hadi hapo
itakapoamuliwa vinginevyo.
itakapoamuliwa vinginevyo.
2.
TEF imechukua uamuzi huo baada ya kupokea
na kujadili kwa kina taarifa ya Kamati ndogo ya wahariri watatu ambayo
iliongozwa na Mhariri wa Nipashe, Jesse Kwayu kwa ajili ya kuchunguza habari
iliyochapishwa na Gazeti la Mtanzania, Jumatano Aprili 17 mwaka huu ikiwa na
kichwa kisemacho “Mtandao Hatari”.
3.
Habari hiyo iliwataja wahariri wawili,
Ansbert Ngurumo wa Tanzania Daima na Deodatus Balile wa Jamhuri kuwa ni
washirika wa Joseph Ludovick, mshitakiwa
katika kesi ambayo ilikuwa ikihusishwa na ugaidi (kabla ya kubadilishwa na
mahakama) lakini ikiwahusisha kwa namna moja au nyingine na tukio la kuumizwa
kwa Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda.
4. Yalikuwa ni maoni ya wahariri wengi katika
Mkutano wa April 18, 2013, kwamba habari hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa
kitaaluma, hivyo kuamua kuchunguza habari hiyo na kubaini iwapo kulikuwa na
ukiukwaji wa maadili na misingi ya kitaaluma ya habari.
5.
0 Kamati hiyo pamoja na mambo mengine
ilipaswa kuchunguza yafatayo:
5.1
Kuchunguza mazingira ya kuchapishwa kwa
habari hiyo na kama kulikuwa na msukumo wowote nyuma ya kuandikwa kisha
kuchapishwa kwakwe.
5.2
Kuchunguza chanzo/vyanzo vya habari hiyo na
kubaini kama kulikuwa na ajenda maalum.
5.3
Kuchunguza ushahidi wa tuhuma zilizotolewa
dhidi ya Deo Balile na Ansbert Ngurumo (kama Mullinda) alivyokiambia kikao cha
Aprili 18 kwamba alikuwa na ushahidi way ale aliyoyaandika.
5.4
Kuchunguza na kubaini iwapo habari husika
ilikidhi vigezo vya kitaaluma.
6.
0 Katika uchunguzi wake Kamati ilibaini
yafuatayo:
6.1
Kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa maadili ya
kitaaluma katika mchakato mzima uliowezesha kuandikwa na kuchapwa kwa habari
husika na kwamba habari hiyo haikuwa na sifa wala vigezo vya kihabari.
6.2
Mulinda akiwa Mhariri wa Gazeti la Tanzania
Jumatano, alishindwa kuthibitisha usahihi wa taarifa hiyo na hata alipotakiwa
kutoa ushahidi wa tuhuma dhidi ya wahariri aliowataja hakuweza kufanya hivyo.
6.3
Tangu kuandikwa kwake, kuhaririwa na hadi
kuchapishwa kwa taarifa hiyo, hakukuwa na vikao rasmi vya wahariri ambavyo
kimsingi ndivyo vinavyopaswa kufanya uamuzi kwamba ni habari gani ichapishwe na
kwa vigezo gani.
6.4
Kwamba kulikuwa na nguvu (msukumo) ya ziada katika
kuchapishwa kwa habari hiyo kwani taarifa kwamba habari hiyo ingechapishwa
zilifahamika siku moja kabla ya kuchapishwa kwa habari yenyewe.
6.5
Kwamba Mhariri
husika alithibitika kukaidi uamuzi wa TEF kwa kuendeleza mjadala huo katika
Makala yake ya Mchokonozi ya Mei 8, 2013 iliyobeba kichwa cha Habari
"Simba hapigani na Binadamu" huku akijua kuwa kufanya hivyo ni
kuingilia Uhuru wa Kamati iliyokuwa ikiendelea na uchunguzi wa suala hilo.
7. 0 Hitimisho
7.1
Kwa
kuzingatia matokeo hayo TEF inaushauri Uongozi wa New Habari (2006) Ltd na vyumba vingine vya habari kuboresha mfumo wake wa usimamizi wa uhariri
ili kuziba mianya kwa habari tata kama hiyo ya "Mtandao Hatari"
kupenya na kuwaumiza baadhi ya watu bila kuwapo kwa uthibitisho wa tuhuma
husika.
7.2
TEF
inaendelea kuchukua hatua nyingine za ndani kuimarisha usimamizi wa nidhamu na
maadili kwa wahariri ikiwa na itaendelea kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji
wowote ule wa kitaaluma utakaofanywa katika vyombo vya habari.
Imetolewa
na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
Dar es
Salaa, Mei 15, 2013
No comments:
Post a Comment