Charles Mullinda
Mhariri Mtanzania Jumatano
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la Wahariri
YAH: KUJITOA KWENYE JUKWAA
Napenda kukufahamisha kuwa nimeamua kujitoa kwenye Jukwaa la Wahariri kwa sababu siridhiki na mwenendo wa Jukwaa hilo.
Nimeamua
kujitoa kwa sababu sijaridhishwa na uamuzi uliofikiwa wa kuingilia
uhuru wa habari na kufumbia macho baadhi ya mambo ambayo ninaamini
hayapaswi
kufumbiwa macho.
kufumbiwa macho.
Uamuzi
wangu huu pia unatokana na jinsi jukwaa linavyotumia nguvu kubwa
kuficha ukweli unao wahusisha baadhi ya wahariri ambao gazeti hili
lilibaini kuwa walikuwa na mawasiliano yenye utata na aliyekuwa
mtuhumiwa wa ugaidi, Joseph Ludovick.
Aidha,
siridhishwi na jinsi baadhi ya wahariri wanavyoshambuliwa na wahariri
wenzao katika magazeti yao pasipo Jukwaa kuchukua hatua huku kwa upande
mwingine likitumia nguvu kubwa na pesa nyingi kuwalinda baadhi ya
wahariri ambao nyendo zao zinatia mashaka.
Kikao
cha kwanza na TEF na kilichofanyika leo kimedhihirisha pasipo mashaka
kuwa TEF iliamua kuwa na ajenda maalumu ya kumshughulikia Mullinda kwa
kuwa tu nilionyesha mawasiliano ya Deodatus Balile na Ansbert Ngurumo
dhidi ya Ludovick kama ambavyo gazeti la Tanzania Daima lilivyoonyesha
mawasiliano ya Dennis Msaki na Ludovick.
Ripoti
ya timu iliyoundwa kuchunguza ukweli wa habari iliyoandikwa na gazeti
la Mtanzania Jumatano ina upungufu mkubwa wa kimantiki ambao hata kwenye
kikao niliuonyesha lakini haukusikilizwa.
Ushahidi
wa Ngurumo kumtuma pesa Ludovick upo wazi, lakini hakuna mtu
anayeliangalia hilo kwa sababu tu timu ile iliundwa kumshughulikia
Mullinda kwa sababu aliandika vigogo wa TEF ambao wako karibu na
viongozi wa TEF.
Nimeamua kujitoa baada ya kubaini kuwa jukwaa linafanya kazi kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi.
Kwa taarifa hii naamini utaratibu wa kawaida wa kuagana utazingatiwa.
Charles Mullinda.
No comments:
Post a Comment