Mwanzoni wa mwaka 2012, kabla dunia haijasikia miwani ya Google,
palikuwa na uvumi mkubwa kwamba kampuni hiyo iko katika mkakati wa kutoka na
miwani ya ajabu.
Siku zilivyo kuwa zinakwenda, ni wazi haukuwa uzushi bali ni
ukweli mtupu, lakini ndoto ya timu ya wataalamu wa Google kutoka na kifaa
kitakachovaliwa kama miwani haikuwa karibu kiasi cha kutoa na kutambulisha
teknolojia hiyo kama watu walivyotarajia.
Lakini kwani ni kitu gani hicho ambacho kinazoa akili za
watu na kusubiri kwa hamu kubwa?
Miwani hii (Pichani) maarafu kama ‘Google Glass’ ni kifaa
ambacho kitakuwa na uwezo wa kufanya kazi kama kompyuta yako ya mezani au simu
au hata ipad, lakini tofauti ni kwamba safari hii itakuwa kwenye macho yako
kama picha inavyoonesha juu.
Kwa urahisi tu, Google Glass ni kamera, kioo kinachoonesha
kama skrini yako ya kompyuta au simu, ina teknolojia ya kugusa kama simu za
siku hizi (touch screen), inatumia betri, na ina kipaza sauti (micrphone) vyote
hivyo vimewekwa ndani ya miwani ili uweze kuona na kufanya vitu ukiwa katika
shughuli zako, kama kuangalia sinema, kupiga picha, kurekodi video, kutafuta
vitu mbalimbali na hata kutafsiri mambo mbalimbali ukiwa unatembea.
Kifaa hicho ambacho kinaongelewa sana sasa hivi kipo katika
majaribio kwa zaidi ya wiki kadhaa sasa. Google inategemea kuuza miwani hiyo
kwa bei ya dola za kimarekani 1,500 nchini marekani, na kuingiza rasmi sokoni
kufikia mwishoni mwa mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment