MFANO WA KIINI KILICHO KATIKA HATUA ZA MWANZO ZA KUKUA (Picha kwa hisani ya SPL)
Kiini tete
cha mwanadamu kilichotumika kuzalisha kiini cha kiumbe cha mwanadamu ambacho
hukua na kutengeneza mtoto ndani ya yai linalokuja kuzalisha mwanadamu kimepuga
hatua kubwa za kikemikali kwa mujibe wa wanasayansi nchini Marekani.
Kondoo Dolly Akinyonyeshwa, kondoo huyo aliyevumbuliwa mwaka 1996 ni mafanikio makubwa kisayansi duniani.
Habari kutoka
katika mitandao mbalimmbali ikiwemo BBC ziliripoti kuwa kiini hicho kimetumia
seli za kupandikiza ambazo zimeweza kutengeneza misuli mipya ya moyo, mifupa,
tishu za ubongo, pamoja na seli nyingine za mwili wa mwanadamu.
Utafiti huo
uliochapishwa kwenye jarida la seli, umetumia njia kama zilizotumika kuzalisha
kondoo maarufu kama Dolly nchini Uingereza miaka ya nyuma.
Watafiti
wamedai vyanzo vingine vya viini hivyo vitakuwa rahisi sana, na vya bei nafuu
na kutokuwa na mikanganyiko. Hata hivyo wanaharakati na wapinzani wamedai ni
kinyume cha maadili ya kiutu na sio sahihi kumtengeneza mwanadamu na kutaka
hatua hizo zisimamishwe mara moja.
Lakini wanasayansi
wamedai kuwa kiini tete ni matumaini makubwa katika ufumbuzi wa matibabu. Kuweza
kutengeneza viini vipya yaweza kusaidia kutibu magonjwa mengi yanayotokana na
mshtuko wa moyo au kutibu magonjwa ya uti wa mgongo.
Mfano wa watoto waliotengenezwa kwa mfumo maarufu kama 'baby clonning'
Yameshakuwepo
na majaribio mbalimbali kwa kutumia
viini tete maarufu kama ‘stem cells’ kutoka katika viungo vya kujitolea ili kutibu vipofu.
viini tete maarufu kama ‘stem cells’ kutoka katika viungo vya kujitolea ili kutibu vipofu.
Kwa maana
hiyo kama seli hizo haziendani na mahitaji ya mwili wa mgonjwa, mwili huzikataa
mara moja. Kitendo ambacho hutafsiriwa kama matatizo ya viini hivyo kwenye
mwili wa mgonjwa.
Utaalamu huo
ulitumika kwa mara ya kwanza mwaka 1996, ambapo kondoo maarufu alietengenezwa
na kuitwa Dolly alikuwa ndie mnyama wa kwanza kutengenezwa.
Sehemu ya
seli ya ngozi ya kondoo mkubwa ilichukuliwa na kupandikizwa ndani ya yai ambalo
lilitolewa vinasaba vyote. Kwa kutumia umeme yai hilo liliweza kusaidiwa
kuendelezwa na hatimaye kutengeneza kiini cha mnyama.
Kwa mujibu
wa wanasayansi, matumizi ya utafiti huo ni kwaajili ya tiba na lengo si
kumtengeneza mwanadamu.
Hata hivyo
kitendo hicho kimepigwa vita na wanaharakati mbalimbali duniani na kusema ni
kinyume na utaratibu wa muumba. Ambapo ni mungu tu ndo mwenye uwezo wa kuumba
na sio maahabara.
Wengine wamedai
uumbaji ni kitu cha kiungu na sio cha kibinadamu. Wako waliounga mkono na
kusema ‘kama una mtoto yuko mahututi hutojali wapi au aina ya tiba inapopatikana’
No comments:
Post a Comment