Monday, May 20, 2013

BREAKING NEWS: RAIS OBAMA KUTEMBELEA TANZANIA MWEZI JUNE




Magazeti mbalimbali katika nchi za Afrika yamekuwa yakiripoti kuhusu ziara ya Rais wa Marekani Barrack Obama katika nchi za Afrika, Tanzania ikiwa ni sehemu ya ziara hiyo.

Barrack Obama anatarajiwa kufanya ziara katika nchi za Afrika kuanzia mwezi ujao ambapo ataanza ziara hiyo nchini Senegal, jijini Dakar.


Kwa mujibu wa gazeti la L’As la Ghana, Rais Obama atafuatana na mkewe Michelle Robinson Obama na watoto wake Malia na Sasha katika ziara hiyo inayotarajiwa kuanza tarehe 26 mpaka 28.

Aidha magazeti nchini Afrika Kusini pia yameandika ziara hiyo ya raisi wa Marekani. Mara ya mwisho Obama kutembelea nchi za jangwa la Sahara ilikuwa ni mwaka 2009 alipotembelea Ghana.

Katika ziara yake, Rais Obama atatembelea Tanzania ambapo kama ilivyo kawaida atapokelewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na baadae kuelekea nchini Rwanda ambapo nchi hiyo imetajwa kuwa na uwezekano mdogo wa kutembelewa.

Mipango ya awali pia imeonesha kuwa Ethiopia imeondolewa katika ziara hiyo, na uwezekano wa Obama kuhudhuria mkutano wa kiuchumi wa U.S.-Sub-Saharan Africa Trade and Economic Cooperation Forum ambapo alipewa fursa ya kuongea imeahirishwa. Jukwaa hilo la kiuchumi limeandaliwa na AGOA ( Africa Growth Opportunity Act)

Nchi nyingine ambazo zinaweza kuondolewa katika ziara hiyo ni pamoja na Nigeria, pamoja na mipango iliyopangwa mwanzo kwamba angepita kwa siku mbili nchini humo, pamoja na maombi ya nguvu ya serikali ya Rais Goodluck Jonahtan na taarifa za vyombo vya habari nchini Nigeria ikiandikwa gazeti la This Day ‘Obama afikiria kupita Nigeria’

KWA MUJIBU WA http://inopstanzania.com/news_detail.php?news=1883



No comments:

Post a Comment