Friday, May 31, 2013

NGWAIR AZIMA NDOTO ZA TID


MSANII wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed 'Tid', amesikitishwa na taarifa ya kifo cha msanii mwenzake Albert Mangwea 'Ngwair' kwa kuwa walikuwa na mpango wakufanya mambo mengi hususani katika swala la muziki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Tid alisema kifo cha msanii huyo kimetokea ghafra huku kikizima ndoto zao ambazo walikuwa wanatarajia kuzifanya ikiwemo kurekodi nyimbo nyingine.


Alisema kuwa alifanya mawasiliano na msanii huyo alipokuwa nchini Afrika Kusini na teyari alishamuahidi kuwa anatarajia kurudi hivi karibuni na kuendelea na taratibu zao za kurekodi nyimbo.

"Mimi na Ngwair tumeweza kusihi muda mrefu kwa sababu tunajuana na tabia yetu ni moja amekuwa zaidi ya rafiki kwangu, tumepanga mengi lakini kifo ndicho kimekwamisha ndoto zetu inaniuma sana tena sana" alisema Tid.

Mwili wa msanii huyo unatarajia kuwasili nchini kesho kutoka Afrika Kusini ambapo utaagwa katika viwanja wa Leaders Club Jumapili na kuzikwa Jumatatu Morogoro



No comments:

Post a Comment