Thursday, May 30, 2013

MWILI WA NGWAIR KUANZA KUFANYIWA UCHUNGUZI LEO


MWILI wa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Albert Mangwea 'Ngwair' umeanza kufanyiwa uchunguzi leo katika hospitali ya serikali ya Hillbrow iliyopo nchini Afrika Kusini ili kubaini chanzo cha kifo chake.

Kwa mujibu wa watu waliokuwepo Afrika Kusini na kushuhudia mwili wa marehemu wanadai kuwa mwili wa msanii huo umeanza kufanyiwa uchunguzi jana mchana na matokeo ya uchunguzi huo yatakabidhiwa kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo nchini humo.


Taarifa hizo zilidai kuwa zinahitajika zaidi ya shilingi milioni nne na nusu kwa ajili ya kuusafirisha mwili wa marehemu Ngwair, ingawa baadhi ya watanzania wanaoishi nchini humo wanakaa vikao kwa ajili ya kuangalia taratibu za kuusafirisha mwili wa msanii huyo.

Kwa mujibu wa kaka wa marehemu Kenneth Mangwea alisema baada ya kumaliza uchunguzi huo ndipo mwili wa marehemu utasafirishwa kuja Tanzania siku ya Jumamosi.

No comments:

Post a Comment