Viongozi wawili kutoka Manchester United -- Anthony Benerjee, Mkurugenzi wa
Uhusiano na Michael Higham, Meneja Uhusiano – wanatua jijini Dar es Salaam
Jumatano hii kufanya manzungumzo na viongozi wa Airtel Tanzania namna bora ya
kuendesha michuano ya vijana chini ya
umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu.
umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni moja ya wadau
wataoshiriki mkutano huo ili kutoa mchango wao hasa katika masuala ya kifundi
kama vile upangaji wa ratiba ya mashindano. Ratiba ya kuanza kwa ARS 2013
inatarajiwa kutangazwa mwezi huu.
Michuano ya soka Airtel Rising Stars ilizinduliwa hapa
nchini Tanzania na sehemu nyingine barani Afrika mwaka 2011 ikiwa na lengo
mahsusi la kusaidia kuvumbua vipaji vya wanasoka chipukizi na kuwafanya
waonekane kwa makocha na mawakala wa kusaka vipaji vya wachezaji nyota.
Mashaindano haya huanzia ngazi ya chini ambapo timu za
sekondari ngazi ya mkoa huchuana ili kupata wachezaji nyota wa kuunda kombaini inayowakilisha
mkoa husika kwenye mashindano ya Taifa ambayo hufanyika jijini Dar es Salaam.
Jumla ya timu 48 zimepata fursa ya kushirikia
ARS katika miaka miwili iliyopita.
ARS katika miaka miwili iliyopita.
Katika mwaka wa uzinduzi 2011 mashindano ya ARS ngazi
ya Taifa yalifuatiwa na kliniki ya kimataifa chini ya usimamizi wa makocha kutoka
Manchester United iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kushirikisha wavulana na wasichana kutoka nchi za Kenya,
Malawi, Sierra Leone na mwenyeji Tanzania.
No comments:
Post a Comment