Friday, May 17, 2013
BREAKING NEWS: BARNABA AKANUSHA KUFUKUZWA THT
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Barnaba Elias 'Barnaba Boy' akanusha taarifa ambazo zimezagaa
kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii juu ya kufukuzwa kwenye Nyumba ya Kukuza Vipaji (THT) akiwemo na msanii mwenzie Linah Sanga 'Linah', kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Taarifa hizo za kufukuzwa THT zimeibuka
baada ya wasanii hao hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady Jay Dee ingawa walikuwa tayari wameshachukua malipo ya awali ya tamasha hilo linayotarajia kufanyika Mei 31 jijini Dar es Salaam.
Barnaba alisema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na hakuna jambo hilo la wao kufukuzwa wala kupewa adhabu yoyote.
"Habari si za kweli wala hakuna ukweli wa jambo hilo hakuna kikao kilichofanyika kutoka kwa viongozi wetu kutujadili sisi kufukuzwa hivyo waache habari za uzushi" alisema Barnaba
Akizungumzia sababu ya wao kujitoa kwenye shoo hiyo ya miaka 13 ya Jay Dee alisema kuwa walishindwa kukubaliana malipo kwa pande zote mbili.
"Hatukukubaliana kwenye malipo hela ambayo mimi nilikuwa naitaka wameshindwa kufika kwenye kiwango hicho, hiyo kwangu ndiyo sababu na siwezi kuendelea kuzungumzia hilo swala nimeshasema hivyo ibaki hivyo hakuna jambo lingine" alisema Barnaba
Barnaba pamoja na Linah ni kati ya wasanii wa kwanza kujitokeza kukubali kushiriki katika shoo ya uzinduzi wa albamu ya Jay dee ambayo pia ni maalum ya kutimiza miaka 13 ya msanii huyo, ingawa sasa wamejitoa rasmi na kurudisha malipo ya awali ambayo walikwisha pokea.
Kwa upande wake Meneja wa Jay Dee ambaye pia ni mumewake Gadna G. Habashi alisema kuwa alipkea taarifa ya kutokewapo tena kwenye shoo hiyo ingawa sababu hazikuwekwa wazi
Alisema baada ya kutoa taarifa hiyo walifwataa utaratibu na kurudisha malipo ya awali ambayo teyari walishayapokea hapo mwanzo kwa ajili ya shoo hiyo
"Barnaba alirudisha fedha ambazo hapo mwanzo tulimpa na alishafanya matangazo ya kuwepo kwenye shoo hiyo ila nashangaa kupokea taarifa yake ya kutokuwepo ingawa sababu yake haikuwekwa wazi sana " alisema Gadna
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment