Friday, May 17, 2013

WIZI MKUBWA WATIKISA TAMASHA LA FILAMU


Vito vyenye thamani ya zaidi dola za Kimarekani milioni moja sawa na zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 1.6, vimeibiwa  katka eneo la Cannes huko Ufaransa
, polisi wamedai.
Kwa mujibu wa BBC vito hivyo vilikuwa vinaandali kwa ajili ya watu maarufu waliofika katika mji huo kwaajili ya tamasha kubwa linalofanyika kila mwaka la filamu maarufu kama Cannes Film Festival.
vito hivyo viliripotiwa kuibiwa kutoka katika sefu ya chumba cha mwajiriwa mmoja kutoka duka la Uswizi lijuliknalo kama Chopard. Tamasha hilo limefunguliwa jumatano ya wiki hii ambapo kwakiasi kikubwa washiriki wengi wanatarajia makubwa kutoka kwenye sinema mpya ya The Great Gatsby


No comments:

Post a Comment