Wednesday, June 13, 2012

WATUMISHI WANAOUZA DAMU WAPEWA ONYO

 Na mwandishi wetu

KAIMU Meneja Ofisi Viwango na Ubora wa Damu Salama, Bw Ndeonasia Towo, amekemea vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu kuuza damu hali inayosababisha wananchi kutokushiriki kujitolea damu kwa hiari.

Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, Bw. Towo alisema hali hiyo inachangia uhaba wa damu.

"Hivi kweli leo hii mwanachama anachangia damu bure katika benki zetu za damu, kesho inatokea anaumwa au ndugu yake ni mgonjwa anaambiwa alipie damu kesho hawezi kurudia kuchangia,"alisema Bw.Towo.

Bw. Towo aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wahisani ndiyo wadhamini wakuu na watayarishaji wa damu na kila chupa moja baada ya kutolewa na wananchi utarishaji wake hadi kuhifadhi gharama zake ni kubwa.

Aliongeza kuwa mara baada ya vituo vya hifadhi ya damu salama kutayarisha damu hiyo hutolewa bure kwa hospitali na vituo vya afya vyote vinavyostahili.

Aliwataka wananchi kupambana na vitendo hivyo kwa kuwachukulia hatua wale wanaowatoza fedha kwa ajili kuchangia damu, kwani hali iliyopo ni mbaya wahitaji ni wengi.

Wakati huo huo, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia mpango wa taifa wa damu salama umewataka wananchi kujitokeza katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani 14, Juni mwaka.



No comments:

Post a Comment