Wednesday, March 19, 2014

BREAKING NEWS : AJALI YA BASI LA MANING NICE NA BODABODA YAUA WAWILI LEO

Taarifa zilizotufikia leo zimesema kuwa ajali mbaya imetokea leo mchana na kusababisha watu 2 waliokuwa kwenye bodaboda kupoteza maisha na wengine 18 kujeruhiwa huku ikidaiwa kuwa hali zao sio mbaya sana.

Katika ajali hiyo ambayo imedaiwa kuwa chanzo chake ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi la kampuni ya Maning Nice lenye usajili T624CQD aina ya Chong Tong, basi hilo linafanya safari kutoka Dar Es Salaam kwenda Mtwara alishindwa kukwepa pikipiki iliyokuwa imebeba wanaume wawili, kuwagonga na kufariki hapo hapo.

Ajali hiyo ilitokea leo saa 7.30 mchana katika kijiji cha Ngongo, Manispaa ya Lindi Mjini, Mkoa wa Lindi wakati basi hilo likielekea Mtwara.




No comments:

Post a Comment